ARNEL Tinampay raia wa Ufilipino tayari ametua nchini kwa ajili ya pambano lake na Mtanzania, Idd Pialali huku akitamka wazi mpinzani wake ana uwezo mkubwa wa kutembea ndani ya ulingo lakini haiwezi kumtisha.
Bondia huyo
amewasili nchini leo Jumamosi kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya pambano
hilo litakalopigwa Novemba 28, mwaka huu kwenye Ukumbi wa Next Door Arena
uliopo Masaki jijini Dar.
Pambano hilo
ambalo linadhaminiwa na Gazeti la Spoti Xtra, +255 Global Radio, DSTV, Plus TV,
Uhuru Fm, Clouds Media, Precision Air, Smart Gin na Kebby Hotel.
Tinampay amesema kuwa amekuja nchini kwa kazi
moja ya kuhakikisha anampiga Pialali mbele ya Watanzania huku akikiri mpinzani
wake ana uwezo mkubwa wa kutembea ndani ya ulingo jambo ambalo anapaswa kuwa
nalo makini.
"Hii ni
mara ya pili kuja hapa, nimecheza na Mwakinyo (Hassan) yeye alikuwa bora kwa
sababu ya ngumi zake zina nguvu lakini sasa nataka kumpiga Pialali mbele ya
mashabiki wake wa hapa.
"Pialali
ni bondia mzuri, nimeangalia baadhi ya mapambano yake nimeona kwamba anajua
sana na mzuri wa kutembea ulingoni akiwa ana pambana lakini hilo haliwezi
kunitisha kabisa kwa sababu nimejiandaa vizuri,"alisema Tinampay.
Kwa upande
wa tiketi za pambano hilo zinauzwa kwa Sh 20000 mzunguko, Sh 5000 kawaida na Sh
100,000 kwa VIP huku zikipatikana kupitia Nilipe App, maduka ya Vunja Bei Store
na Vunja Bei Toto Sinza, Shishi Food
(Kinondoni), pia Cake City ya
Salasala.
Sehemu nyengine ambazo tiketi zitakuwa ni Kaites Lounge ambayo inapatikana Tabata na
Dickson Sound ya Magomeni.
Mbali
ya pambano hilo mapambano mengine ya utangulizi ambapo Adam
Chiga anatarajia kucheza dhidi ya Adam Kipenga wakati Ramadhan Shauri
akitarajia kucheza dhidi ya Salehe Mkalekwa.
Lakini mkongwe Japhet Kaseba yeye atakata
ubishi na mkali mwingine Iman Mapambano, Seleman Kidunda kutoka Jeshi la Ulinzi
la Wananchi wa Tanzania ‘JWTZ’ yeye
ataonyesha ubavu na mkongwe Said Mbelwa wakati Ismail Galiatano kutoka pia JWTZ
atazichapa na Mustafa Doto.
Kwa upande wa kinadada bondia Stumai Muki
atamaliza ubishi dhidi ya mkali Lulu Kayage.
0 COMMENTS:
Post a Comment