November 30, 2020


 KIKOSI cha Biashara United, wanaopenda kujiita Wanajeshi wa mpakani leo Novemba 30 wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Karume.


Biashara United chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza imekubali kugawana pointi mojamoja na Azam FC.

Azam FC inabidi wajilaumu wenyewe kwa kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa leo kwa kuwa walianza kufunga dakika 20 kupitia kwa Ayoub Lyanga.


Bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili ambapo Biashara United iliweka usawa dakika ya 58 kupitia kwa Thomas Omwenga aliyepiga shuti kali akiwa nje ya 18.


Sare hiyo inafanya Azam FC kufikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 13 ikiwa nafasi ya tatu na Biashara United inafikisha jumla ya pointi19 baada ya kucheza mechi 13.


Pia Biashara United ilikosa penalti kupitia kwa Leen Kissu ambaye amesema kuwa ilikuwa bahati mbaya.

2 COMMENTS:

  1. Sare hiyo inafanya Azam FC kufikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 13 ikiwa nafasi ya tatu
    ..........................

    Azam haiko nafasi ya tAtu,iko nafasi ya pili, rudia maandiko yako kabla hujapost

    ReplyDelete
  2. Ofcause Azam wapo nafasi ya pili huku baba lao Yanga akiwa kileleni mwa msimamo

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic