November 30, 2020




TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo Novemba 30 imetinga hatua ya fainali ya mashindano ya Cecafa kwa mbide baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sudani Kusini.


Mchezo wa leo ambao umechezwa Uwanja wa Black Rhino Academy Karatu ulishuhudia dakika 45 timu zote mbili zikienda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo zikiwa zimetoshana nguvu.


Iliawachukua Ngorongoro Heroes dakika 10 kupata bao la uongozi kupitia kwa Kassim Haruna aliyepachika bao hilo dakika ya 55 baada ya beki wa Ngorongoro, David Kameta kutoa pasi kati iliyokutana na Kelvin John aliyeachia shuti likakutana na kipa aliyetema mpira uliokutana na Haruna.


Mchezo wa leo ulikuwa ni wa nguvu nyingi kwa kuwa Sudani Kusini walikuwa wakitumia nguvu nyingi mwanzo mwisho jambo lililosababisha kushuhudia kadi nyekundu kwa beki Wayiluki ambaye alionyeshwa kadi ya kwanza ya njano dakika ya 23 na ya pili dakika ya 87 iliyolazimu kuonyeshwa kadi nyekundu.


Nyota mwingine wa Sudani Kusini aliyeonyeshwa kadi ya njano ni Khamis Atari dakika ya 30 na kwa upande wa Tanzania ni Pascal Msindo dakika ya 34 alionyeshwa kadi ya njano.


Ushindi huo wa Ngorongoro utaikutanisha na Uganda hatua ya fainali inayotarajiwa kuchezwa Desemba 2, Uwanja wa Black Rhino.


Uganda ilishinda mabao 3-1 dhidi ya Kenya kwenye nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Black Rhino mapema saa sita mchana.


0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic