November 22, 2020

 




TAARIFA kutoka Bodi ya Ligi leo Novemba 22, imeeleza kuwa Kocha Mkuu wa Mwadui FC, Khalid Adam amefungiwa kuiongoza timu yake katika michezo miwili kwa kosa la kukataa kufanya mahojiano na Wanahabari mara baada ya mchezo dhidi ya Simba, Uwanja wa Uhuru.


Mchezo huo Mwadui FC ilipoteza kwa kufungwa mabao 5-0 jambo lililopelekea Adam kugoma kuzungumza.



Pia mbali na hiyo kupitia kikao hicho cha Bodi ya Ligi Kuu Tanzania,(TPLB) kilichofanyika Novemba 20,2020 pia Yanga nayo imepewa adhabu kutokana na mashabiki kuwapiga mawe na chupa waamuzi wa mchezo kati ya Gwambina 0-0 Yanga, Uwanja wa Gwambina Complex.

Taarifa hiyo ipo hivi:-








6 COMMENTS:

  1. Mwadui wamepewa adhabu kwenye mechi na Simba.Je Kagera nae ameadhibiwa kwenye mechi na Simba au Mtibwa?
    Wacheni missleading headlines.
    Makanjanja mnapoteza hadhi yenu tu.

    ReplyDelete
  2. Tunataka taarifa ya waamuzi waliochezesha mechi ya simba simba na yanga

    ReplyDelete
    Replies
    1. Hii itasaidia kupata uelewa mpana wa Sheria 17 za Mpira wa Miguu hasa sisi wa Nje ya Uwanja. Tunahitaji kupata Majibu ya Mchezo huu mapema kabla ya Marudiano ya Watani wa Jadi.

      Delete
  3. Bodi ya ligi inajizimua hawatoi adhabu kwa zile issues ambazo zingeendeleza mpira wetu bali wanafanya usanii, waamuzi ndo wanaovuruga mpira wetu kila mtu anaona ila hakuna adhabu zinazotolewa kwao anapewa adhabu ambae kachoka kuzungumza ni usanii tu, marefaree na mkuu wao hawa ndo wanaotuvurugia mpira wetu, TFF fanyeni kweli chukueni hatua za ukweli ili tuone kama kweli kuna nia ya kuendeleza soka letu.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Bado tuna imani na Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF).

      Delete
  4. Mchezo wa yanga na simba ni makosa ya kibinadamu, hakuna var huku.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic