LEO Uwanja wa Mkapa kuna vita
mpya ya kusaka rekodi ndani ya Uwanja wa Mkapa kwa wanaume 22 ambao watashuka
uwanjani kusaka pointi tatu muhimu.
Namungo 2019/20 ilishiriki kwa
mara ya kwanza Ligi Kuu Bara ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery ambaye
alifutwa kazi Novemba 18 na mikoba yake ipo chini ya Kocha Mkuu, Hemed Morocco.
Jumla yalipatikana mabao sita,
Yanga ikifunga mabao matatu na Namungo pia ilifunga mabao matatu. Walipokuwa
wakisaka pointi sita kila mmoja waliambulia pointi mbili.
Mchezo uliochezwa Uwanja wa
Mkapa, Yanga ililazimisha sare ya kufungana mabao 2-2 na Yanga ilipoibukia
Uwanja wa Majaliwa Lindi ililazimisha sare ya kufungana bao 1-1.
Rekodi mpya
Leo wanakutana Uwanja wa Mkapa kwa mara nyingine tena kila timu ikiwa inahitaji kuweka rekodi mpya ya kusepa na pointi tatu jumlajumla ndani ya uwanja kwa kuwa hakuna ambaye aliweza kufanya hivyo msimu uliopita.
Yanga inaingia uwanjani ikiwa na
kocha mpya ambaye ni Cedric Kaze ambaye alichukua mikoba ya Zlatko Krmpotic
aliyefutwa kazi Oktoba 3 na Namungo pia inainga uwanjani ikiwa chini ya Hemed
Morroco ambaye amechukua mikoba ya Thiery.
Kaze kuhusu mchezo huo alisema
:-”Ni mchezo mgumu na utakuwa na ushindani mkubwa, ninatambua kwamba ni timu
imara na inaleta ushindani ndani ya uwanja ila nimewapa wachezaji wangu mbinu
za kupambana,” .
Morroco wa Namungo
alisema:”Maandalizi na kila kitu kuhusu mchezo kimekamilika ni suala la
kusubiri wakati ili kuona namna gani tutakipata kile ambacho tunakitafuta
ambacho ni pointi tatu,” .
Safu ya ulinzi
Zote zikiwa zimecheza mechi 10,
Yanga ni imara kwenye upande wa ulinzi ambapo imeruhusu mabao ya kufungwa
matatu huku Namungo ikiwa imefungwa mabao saba.
Safu ya ushambuliaji
Yanga safu yake imefunga mabao 12 na kinara wa ufungaji ni Michael Sarpong mwenye mabao matatu na kwa Namungo wao wamefunga mabao saba na kinara wa utupiaji ni Bigirimana Blaise mwenye mabao manne.
0 COMMENTS:
Post a Comment