November 22, 2020

 


NEWCASTLE United ikiwa Uwanja wa St James Park ilikubali kuyeyusha pointi tatu mazima baada ya kukubali kichapo cha mabao 0-2 dhidi ya Chelsea. 


Chelsea chini ya Kocha Mkuu Frank Lampard ilianza kwa kasi jana Novemba 21 kulisakama lango la wapinzani hali iliyopelekea Federico Fernandez beki wa Newcastle United kujifunga dakika ya 10.


Kipindi cha pili Chelsea ilizidi kupambana na iliweza kupata bao la pili dakika ya 65 kupitia kwa Tammy Abraham akipokea asisiti ya Timo Werner.


Ushindi huo unaifanya Chelsea kufikisha jumla ya pointi 18 sawa na Leicester City ambayo itashuka uwanjani leo kumenyana na Liverpool wenye pointi 17.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic