November 18, 2020


 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kukosekana kwa nyota wake Gerson Fraga kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United ya Nigeria kumetibua mipango yake.


Fraga kwa sasa anatibu jeraha la goti ambalo alipata kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Biashara United atakuwa nje kwa muda mrefu kabla ya kurejea uwanjani.

Simba ina kazi ya kusaka tiketi ya kutinga hatua ya makundi kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika ambapo mchezo wa awali itaanza kumenyana na Plateau United ya Nigeria kati ya Novemba 27-29.


Sven raia wa Ubelgiji amesema:-"Alikuwa kwenye mpango wa kikosi changu na ni mchezaji ambaye alikuwa akitimiza majukumu yake vizuri ila nitamkosa kwenye mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo ule mpango wa kwanza umekwama.

"Hatutakuwa naye kwenye mchezo wetu ambao utakuwa na ushindani mkubwa hiyo ni hasara kwetu hivyo tuna kazi ya kumtafuta mbadala wake haraka,".



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic