GARETH Bale nyota wa Klabu ya Tottenham Hotspurs ambaye ni nahodha wa timu ya Taifa ya Wales amesema kuwa amefurahi kurejea kwenye timu yake ya zamani jambo ambalo linampa furaha.
Bale mwenye umri wa miaka 31 aliibukia ndani ya Real Madrid msimu wa 2013 akitokea Klabu ya Totenham ambapo huko alicheza jumla ya mechi 146 na alifunga mabao 42 na akiwa ndani ya Real Madrid alicheza jumla ya mechi 171 na kutupia mabao 80.
Winga huyo kwa sasa amerejea ndani ya klabu yake ya zamani kwa mkopo na tayari amecheza mechi tatu na kufunga bao moja jambo ambalo linampa matumaini kocha wake Jose Mourinho kwamba atafanya vizuri zaidi.
Bale amesema kuwa anafuraha kubwa kurejea ndani ya timu yake hiyo kwa kuwa ni sehemu ambayo alikuwa anaipenda kwa muda mrefu hivyo atapambana kufikia malengo yake.
"Ninajisikia vizuri kuwa ndani ya Tottenham na kurudi kwangu ninaona kuna mafanikio hasa ukizingatia kwamba hii ni sehemu ambayo ninaipenda na nina amini nitafanya vizuri zaidi na nitacheza kwa juhudi kwa kushirikiana na wachezaji wenzagu kwa ajili ya timu yetu," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment