KOCHA Msaidizi wa Gwambina, Athuman Bilali ‘Bilo’ amesema timu yake haitatoa likizo kwa wachezaji wake kwakuwa malengo ya timu yake ni kurekebisha makosa yanayojitokeza kwenye timu hiyo ili waweze kupata matokeo kwenye michezo ya ligi kuu.
Bilali ambaye ni kocha wa zamani wa
Stand United amesema “:Kama benchi la ufundi la Gwambina tumeamua kutotoa
mapumziko yoyote kwa wachezaji wetu tumepanga mazoezi yetu kuendelea katika
kipindi hiki cha mapumziko na sisi tutaendelea kupambana mpaka mwisho.
“Kwenye michezo miwili ambayo
tumecheza kwenye uwanja wetu wa nyumbani mmoja tumefungwa bao 3-0 na KMC na
mwingine tukapata sare ya bila kufungana na Yanga, kiufundi timu yetu bado
tunafanya makosa mengi ambayo tunatakiwa kuyapunguza tukiwa mazoezini.
“Hivyo naamini kwamba ligi ikirejea tutafanya
vizuri zaidi kwakuwa makosa yatakuwa yamepungua.
“ Nawaomba wapenzi na mashabiki wa
Gwambina waendelee kuisapoti timu yao kuhakikisha inafanya vizuri na sisi kama
viongozi wa benchi la ufundi tutaendelea kupambana na kufanya mabadiliko
makubwa,” amesema Bilal.
0 COMMENTS:
Post a Comment