November 27, 2020


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa beki wao wa kulia mwenye jukumu la kumwaga mipira kati kwa sasa anaendelea vizuri baada ya kuumia bega.


Kibwana ambaye ni mrithi wa viatu vya Juma Abdul alipata maumivu hayo Novemba 25 Uwanja wa Azam Complex wakati timu yake ya Yanga ikiubuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC.


Nyota huyo mwenye pasi moja ya bao kati ya mabao 14 yaliyofungwa na Yanga ni chaguo la Kwanza la Cedric Kaze ambaye ni Kocha Mkuu wa Yanga.


Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa maendeleo ya wachezaji yapo sawa ikiwa ni pamoja na Kibwana.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic