MOHAMED Hussein, maarufu kama Mmachinga mshambuliaji wa zamani wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars na mchezaji wa zamani wa Klabu ya Yanga amesema kuwa Simba wanatakiwa kupambana kwa hali na mali kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Jumapili ili kuongeza hali ya kujiamini.
Akizungumza na Saleh Jembe, Mmachinga amesema kuwa wawakilishi hao wa kimataifa wanakutana na mtihani mgumu wakiwa ugenini kutokana na asili ya mpira wa Afrika kuwa mgumu kwa mechi za ugenini.
"Ukizungumzia mechi za ugenini siku zote kwa bara la Afrika zinajulikana kwamba huwa zinakuwa ngumu hivyo wanachotakiwa kukifanya wawakilishi wetu ni kupambana kupata matokeo chanya.
"Kila mmoja anatambua kwamba kuna ugumu wa kupata matokeo kwani wapinzani wao Plateau United sio timu nyepesi lakini ni lazima wajiamini na wapambane kusaka ushindi inawezekana.
"Kikubwa maandalizi mazuri na kuingia kwa tahadhari wasifikiri watakuwa nyumbani hapana kule ni ugenini, kila timu inahitaji matokeo ila matokeo mazuri kwa Simba itakuwa zawadi kwa mashabiki wa Tanzania kiujumla," amesema.
Novemba 29 Simba itakuwa Uwanja wa New Jos kusaka ushindi mbele ya Plateau United ikiwa ni mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika, ikimalizana nao Nigeria itakutana nao Bongo kwenye mchezo wa marudio kati ya Desemba 4-6.
0 COMMENTS:
Post a Comment