STAA wa Bongo Fleva, Rajabu Abdul Kahali ‘Harmonize’, amevunja rekodi ya msanii mwenzake, Ali Saleh Kiba ‘King Kiba’ aliyoiweka miaka mitatu iliyopita.
Kupitia wimbo wake mpya wa Ushamba, Harmonize au Harmo amefunika rekodi iliyowekwa na kushikiliwa kwa muda mrefu na Wimbo wa Seduce Me wa Kiba kwenye Mtandao wa YouTube.
Wimbo huo wa Ushamba umeweka rekodi ya kusikilizwa na kutazamwa mara zaidi ya milioni 2 ndani ya saa 48. Rekodi kama hiyo iliwekwa na Wimbo wa Seduce Me mwaka 2017.
Kwa upande wake, Wimbo wa Ushamba umevunja rekodi ya video zote za wasanii nchini Tanzania na Afrika Mashariki kwa kusikilizwa na kutazamwa mara nyingi zaidi ndani ya saa 48 (siku mbili). Video hiyo ambayo iliachiwa rasmi Novemba 8, mwaka huu, imeendelea kushikilia nafasi ya kwanza kwenye orodha ya video zote zinazotrendi Tanzania na Kenya.
Rekodi nyingine ambayo pia imevunjwa na Wimbo wa Ushamba ni ile iliyowekwa na video ya Wimbo wa Salome wa msanii Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ akishirikiana na Raymond Mwakyusa ‘Rayvanny’ ambao ulitazamwa mara zaidi ya milioni moja ndani ya saa 48.
Hata hivyo, kuna kila dalili kuwa Wimbo wa Ushamba ukaendelea kupata watazamaji wengi zaidi kutokana na jinsi unavyoendelea kutazamwa kwa kasi ya ajabu. Kwa wastani, ndani ya dakika moja, video hiyo kwa sasa inatazamwa zaidi ya mara 1,000 duniani kote kupitia YouTube.
Ushamba ni wimbo uliokuwa unasubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Harmo kutokana na promo kubwa iliyopigwa huku Harmonize akiwa hajaachia wimbo mpya kwa miezi kadhaa.
.
Nini hiki umeweka!
ReplyDeleteUongo mtupu.
Ngoma ina wiki nzima sasa
ReplyDeleteNaona Sasa hii blog imekuwa ya kiswazi ni full umbea tu... Mtapoteza wadau asee na mimi nikiwemo
ReplyDelete