November 25, 2020

 


UNAUKUMBUKA ule mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa zama zile ukiitwa Uwanja wa Taifa kati ya Yanga na Azam FC msimu uliopita?

Juni 21,2020 ipo kwenye kumbukumbu kutokana na matokeo tata ambayo yalitokea baada ya dakika 90 kukamilika kutokana na timu zote kutoshana nguvu ya bila kufungana.

Achana na matokeo kwamba ilikuwa ni sare na timu zote ziligawana pointi mojamoja bila kufungana suala kubwa ilikuwa ni kwenye maamuzi ambayo wengi walionekana wakilalamikia.

Ikumbukwe kuwa Azam FC iliandika barua Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kuhusu maamuzi ya waamuzi waliochezesha mchezo huo kwa kuwa waligomea mabao mawili ya Azam FC ambayo waliamua kwamba wafungaji walikuwa wameotea.

Basi leo tena ni siku nyingine mzunguko wa kwanza wababe hawa wanakutana Uwanja wa Azam Complex kusaka pointi tatu muhimu, jambo la msingi ni kila mmoja kutimiza majukumu yake.

Ishu ya dakika 90 kukamilika na watu kuanza kuingia ofisini na barua za malalamiko hii sio sawa kwani makosa yanaweza kurekebishika na ushindi ukapatikana.

Nina amini kwamba kila mmoja anahitaji kuona timu inapata ushindi tena wa haki na inawezekana ikiwa kila mmoja atatimiza wajibu wake.

Tupo kwenye msimu mzuri kwa 2020/21 hasa ukizingatia kwamba kila timu inapambana kutafuta ufalme wake ndani ya ardhi ya Bongo.

Waamuzi kazi kwenu kutimiza majukumu yenu na wachezaji kazi kwenye kupambana kusaka matokeo ndani ya uwanja.

Maandalizi mazuri yanahitajika ili timu ipate ushindi ndani ya uwanja na kila timu kwa namna ambavyo itajipanga ina nafasi ya kushinda. 

Wachezaji mna kazi ya kukumbuka kwamba tayari raundi 11 zimemeguka jumlajumla na sasa raundi ya 12 nayo inakwenda ukingoni taratibu.

Huu ni mzunguko wa 12 ambao kila timu ina nafasi ya kupata kile inachostahili ndani ya uwanja. Yale yaliyopita mzunguko wa 11 lazima yafanyiwe kazi kwa upade wa makosa.

 

Kazi kubwa kwa kila timu ipo kwenye kusaka ushindi. Zipo ambazo zinakwenda mwendo wa kobe ndani ya uwanja hilo linapaswa lifanyiwe kazi mapema kwa sasa.

 

Hesabu ambazo zinapigwa wakati huu zitajibiwa mwisho wa msimu, timu ambayo inaona haielewi inavyokwenda ikifika mwisho itapata picha ya kile ilichokuwa inapambania ndani ya uwanja.


Ipo wazi matokeo yapo yale ya aina tatu ikiwa ni ushindi, kupoteza ama kupata sare. Mwenye maamuzi ya aina ya matokeo wanayotaka ni benchi la ufundi lenyewe.

Ikiwa litafanya maandalizi mepesi na matokeo yatakuwa mepesi pia ndani ya uwanja, ikiwa maandalizi yatakuwa mazuri nje ya uwanja na ndani ya uwanja ni jukumu lao kupata matokeo mazuri.

Hakuna ambaye anapenda kuona timu inaboroga ndani ya uwanja kwani matokeo mabovu yanaumiza kwa wachezaji na mashabiki pia.

 

Ili kuweza kufikia matokeo hayo ni lazima kila mmoja aonyeshe juhudi zake. Benchi la ufundi likifanya yanayostahili kwa wakati huku wachezaji nao wakitimiza majukumu yao kwa wakati ni mwanzo wa ushindi.

 

Makosa ambayo yameonekana kwenye mechi ambazo zimepita benchi la ufundi ni lazima lifanyie kazi na kuweka kando sababu ambazo hazina maana.

Ni wazi kwamba mashabiki huwa hawaelewi ukija na sababu nzuri na za msingi kuhusu kushindwa kupata ushindi wao wanahitaji ushindi kwenye kila mechi.

 

Hili ni gumu kuweza kutokea kwenye mechi zote kwani tunaona hata kwa timu za ulaya namna zinavyopambana kupata matokeo ndani ya uwanja.

 

Wakati tunaitazama Ligi Kuu Bara tusiiweke kando pia Ligi Daraja la Kwanza katika kufuatilia na kuona namna gani mambo huku yanakwenda.

 

Ninapenda kusema kwamba huku Ligi Daraja la Kwanza ni hazina ya wachezaji wa kesho kwa zile timu ambazo zitapanda ligi.

Zina nafasi kubwa ya kutengeneza kizazi cha dhahabu ambacho kitaleta ushindani mkubwa kwa msimu ujao hivyo ni muhimu kutazama maisha yao namna yanavyokwenda.

Wimbo wao siku zote ni kuhusu ishu ya wadau kuwapa sapoti kwenye upande wa uendeshaji hivyo kwa yule mwenye uwezo wa kuzishika mkono timu hizi ni muhimu akafanya hivyo.

Ugumu upo kwenye kusaka matokeo ndani ya uwanja na kila timu inapambana kusaka ushindi katika hili hakuna kukata tamaa licha ya mazingira kuwa magumu.

Wadau tusijisahaulishe tuwakumbuke hawa ndugu zetu pia kwenye Ligi Daraja la Kwanza kwa kuwa wanauwezo mkubwa wa kutupa burudani na mashabiki ni mtaji wao.

Angalau kidogo kwa sasa ninaona kwamba ile kesi ya ubovu wa viwanja inaanza kupungua taratibu katika hili wahusika mnastahili pongezi.

Tumeona namna Uwanja wa Jamhuri Dodoma ukiwa umeruhisiwa kuanza kufanyiwa matumizi baada ya kufungiwa pia hata ule wa Gwambina Complex nao pia umeanza kutumika muda kidogo.

Kufungiwa kwa viwanja hivi kunapaswa kuwe darasa kwa wakati ujao katika kuzingatia vigezo na masharti ambayo yamewekwa.

Ikiwa kutakuwa na upuuziaji katika utekelezaji ina maana kwamba na wakati ujao pia masuala ya kufungiafungia yataanzia pale ambapo msimu huu yameishia.

Nina amini kwamba mamlaka husika wakati ujao zitakuwa makini katika kutoa vibali kwa viwanja ambavyo vitatumika na itafanya kila mchezaji kuwa na furaha anapokuwa ndani ya uwanja.

Wachezaji ujumbe wenu ni kwamba ni muhimu kupambana ndani ya uwanja kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja jambo ambalo litawafanya muwe ndani ya 10 bora.

Pengine wapo wanaofikiria kutwaa ubingwa basi ni muhimu kwa kila mchezaji kupambana kwa hali na mali kupata matokeo chanya ndani ya uwanja.

2 COMMENTS:

  1. Hapa sawa kabisa tumechoka Na Lawama za waamuzi.

    ReplyDelete
  2. Wewe mwenyewe matokeo ya mechi za FDL hautoi. Uwe unatuwekea matokeo yote ya mechi za FDL.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic