UNAUKUMBUKA ule mchezo uliochezwa Uwanja wa Mkapa zama zile ukiitwa Uwanja wa Taifa kati ya Yanga na Azam FC msimu uliopita?
Juni 21,2020 ipo kwenye kumbukumbu
kutokana na matokeo tata ambayo yalitokea baada ya dakika 90 kukamilika
kutokana na timu zote kutoshana nguvu ya bila kufungana.
Achana na matokeo kwamba ilikuwa ni
sare na timu zote ziligawana pointi mojamoja bila kufungana suala kubwa ilikuwa
ni kwenye maamuzi ambayo wengi walionekana wakilalamikia.
Ikumbukwe kuwa Azam FC iliandika
barua Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) kuhusu maamuzi ya waamuzi waliochezesha
mchezo huo kwa kuwa waligomea mabao mawili ya Azam FC ambayo waliamua kwamba
wafungaji walikuwa wameotea.
Basi leo tena ni siku nyingine
mzunguko wa kwanza wababe hawa wanakutana Uwanja wa Azam Complex kusaka pointi
tatu muhimu, jambo la msingi ni kila mmoja kutimiza majukumu yake.
Ishu ya dakika 90 kukamilika na
watu kuanza kuingia ofisini na barua za malalamiko hii sio sawa kwani makosa
yanaweza kurekebishika na ushindi ukapatikana.
Nina amini kwamba kila mmoja anahitaji
kuona timu inapata ushindi tena wa haki na inawezekana ikiwa kila mmoja
atatimiza wajibu wake.
Tupo kwenye msimu mzuri kwa 2020/21
hasa ukizingatia kwamba kila timu inapambana kutafuta ufalme wake ndani ya
ardhi ya Bongo.
Waamuzi kazi kwenu kutimiza
majukumu yenu na wachezaji kazi kwenye kupambana kusaka matokeo ndani ya
uwanja.
Maandalizi mazuri yanahitajika ili
timu ipate ushindi ndani ya uwanja na kila timu kwa namna ambavyo itajipanga
ina nafasi ya kushinda.
Wachezaji mna kazi ya kukumbuka
kwamba tayari raundi 11 zimemeguka jumlajumla na sasa raundi ya 12 nayo
inakwenda ukingoni taratibu.
Huu ni mzunguko wa 12 ambao kila
timu ina nafasi ya kupata kile inachostahili ndani ya uwanja. Yale yaliyopita
mzunguko wa 11 lazima yafanyiwe kazi kwa upade wa makosa.
Kazi kubwa kwa kila timu ipo kwenye
kusaka ushindi. Zipo ambazo zinakwenda mwendo wa kobe ndani ya uwanja hilo
linapaswa lifanyiwe kazi mapema kwa sasa.
Hesabu ambazo zinapigwa wakati huu
zitajibiwa mwisho wa msimu, timu ambayo inaona haielewi inavyokwenda ikifika
mwisho itapata picha ya kile ilichokuwa inapambania ndani ya uwanja.
Ipo wazi matokeo yapo yale ya aina
tatu ikiwa ni ushindi, kupoteza ama kupata sare. Mwenye maamuzi ya aina ya
matokeo wanayotaka ni benchi la ufundi lenyewe.
Ikiwa litafanya maandalizi mepesi
na matokeo yatakuwa mepesi pia ndani ya uwanja, ikiwa maandalizi yatakuwa mazuri
nje ya uwanja na ndani ya uwanja ni jukumu lao kupata matokeo mazuri.
Hakuna ambaye anapenda kuona timu
inaboroga ndani ya uwanja kwani matokeo mabovu yanaumiza kwa wachezaji na
mashabiki pia.
Ili kuweza kufikia matokeo hayo ni
lazima kila mmoja aonyeshe juhudi zake. Benchi la ufundi likifanya
yanayostahili kwa wakati huku wachezaji nao wakitimiza majukumu yao kwa wakati
ni mwanzo wa ushindi.
Makosa ambayo yameonekana kwenye
mechi ambazo zimepita benchi la ufundi ni lazima lifanyie kazi na kuweka kando
sababu ambazo hazina maana.
Ni wazi kwamba mashabiki huwa
hawaelewi ukija na sababu nzuri na za msingi kuhusu kushindwa kupata ushindi
wao wanahitaji ushindi kwenye kila mechi.
Hili ni gumu kuweza kutokea kwenye
mechi zote kwani tunaona hata kwa timu za ulaya namna zinavyopambana kupata
matokeo ndani ya uwanja.
Wakati tunaitazama Ligi Kuu Bara
tusiiweke kando pia Ligi Daraja la Kwanza katika kufuatilia na kuona namna gani
mambo huku yanakwenda.
Ninapenda kusema kwamba huku Ligi
Daraja la Kwanza ni hazina ya wachezaji wa kesho kwa zile timu ambazo zitapanda
ligi.
Zina nafasi kubwa ya kutengeneza
kizazi cha dhahabu ambacho kitaleta ushindani mkubwa kwa msimu ujao hivyo ni
muhimu kutazama maisha yao namna yanavyokwenda.
Wimbo wao siku zote ni kuhusu ishu
ya wadau kuwapa sapoti kwenye upande wa uendeshaji hivyo kwa yule mwenye uwezo
wa kuzishika mkono timu hizi ni muhimu akafanya hivyo.
Ugumu upo kwenye kusaka matokeo
ndani ya uwanja na kila timu inapambana kusaka ushindi katika hili hakuna
kukata tamaa licha ya mazingira kuwa magumu.
Wadau tusijisahaulishe tuwakumbuke
hawa ndugu zetu pia kwenye Ligi Daraja la Kwanza kwa kuwa wanauwezo mkubwa wa
kutupa burudani na mashabiki ni mtaji wao.
Angalau kidogo kwa sasa ninaona
kwamba ile kesi ya ubovu wa viwanja inaanza kupungua taratibu katika hili
wahusika mnastahili pongezi.
Tumeona namna Uwanja wa Jamhuri
Dodoma ukiwa umeruhisiwa kuanza kufanyiwa matumizi baada ya kufungiwa pia hata
ule wa Gwambina Complex nao pia umeanza kutumika muda kidogo.
Kufungiwa kwa viwanja hivi
kunapaswa kuwe darasa kwa wakati ujao katika kuzingatia vigezo na masharti
ambayo yamewekwa.
Ikiwa kutakuwa na upuuziaji katika
utekelezaji ina maana kwamba na wakati ujao pia masuala ya kufungiafungia
yataanzia pale ambapo msimu huu yameishia.
Nina amini kwamba mamlaka husika
wakati ujao zitakuwa makini katika kutoa vibali kwa viwanja ambavyo vitatumika
na itafanya kila mchezaji kuwa na furaha anapokuwa ndani ya uwanja.
Wachezaji ujumbe wenu ni kwamba ni
muhimu kupambana ndani ya uwanja kusaka pointi tatu muhimu ndani ya uwanja
jambo ambalo litawafanya muwe ndani ya 10 bora.
Pengine wapo wanaofikiria kutwaa
ubingwa basi ni muhimu kwa kila mchezaji kupambana kwa hali na mali kupata
matokeo chanya ndani ya uwanja.







Hapa sawa kabisa tumechoka Na Lawama za waamuzi.
ReplyDeleteWewe mwenyewe matokeo ya mechi za FDL hautoi. Uwe unatuwekea matokeo yote ya mechi za FDL.
ReplyDelete