November 10, 2020

 


MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara, Simba wameweka wazi kuwa hesabu zao kubwa kwa sasa ni kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.


Msimu uliopita Simba ilipokuwa chini ya Patrick Aussems iliishia hatua ya awali kwa kutolewa na UD Songo kwa faida ya bao la ugenini jambo ambalo lilisababisha kibarua cha kocha huyo ambaye aliifikisha hatua ya robo fainali timu hiyo kuota nyasi.


Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hesabu kubwa kwa sasa ndani ya timu hiyo ni kuweza kufanya vizuri kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika.


"Tunakazi kubwa ya kufanya kimataifa hasa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika hivyo tuna amini kwamba wachezaji pamoja na benchi la ufundi watafanya kazi kubwa kufikia malengo.

"Mashabiki watupe sapoti katika hili kwani kufikia mbali huko lazima tuwe nguvu moja na hii ni sera ya Simba na ipo kwenye nembo yetu hivyo kazi kubwa ni kufanya vizuri kimataifa," amesema.

 Simba itakutana na Plateu United ya Nigeria mchezo unaotarajiwa kuchezwa kati ya Novemba 27-29  na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 4-6 Uwanja wa Mkapa.

5 COMMENTS:

  1. Plateu United lazima ikija hapa bongo ipate mashabiki wengi sana, hivyo MISUKULE fc kipigo hakikwepeki labda mtoroke

    ReplyDelete
    Replies
    1. unacoment osolo maulid si yako unaivalia kanzu utaolewa

      Delete
    2. Unafurahisha kweli, alhal, as vital na wengine walipata mashabiki Kama unavyosema lkn walifanywaje na mnyama? na hao kipigo palepale kibawahusu wasgangilieni, nunueni jezi n.k. Mabingwa hatutishwi na kelele.

      Delete
  2. Nyinyi endeleeni kuwahonga marefa ili wawe wanawapa penati inje ya 20

    ReplyDelete
  3. Misukule FC ndo akina nani? Wenzenu wanashiriki ligi ya mabingwa nyie mnawaponda mashabiki wa mama mdogo mbona mnashida kubwa?

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic