November 10, 2020

 


JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Spurs ametaja orodha ya wachezaji wake 11 bora wa muda wote ambao amewahi kufanya nao kazi huku nane kati ya hao akiwataja aliofanya nao kazi ndani ya Klabu ya Chelsea huku majina ya nyota kama Paul Pogba, Sergio Ramos na Zlatan Ibrahimovic yakikosekana.  

Mourinho  alikuwa ndani ya Stamford Bridge  mwaka 2004 na aliweza kufanikiwa kutwaa taji la Ligi Kuu England mara mbili akiwa ndani ya kikosi hicho.John Terry, Ricardo Carvalho naWilliam Gallas hawa amewaweka sehumu ya ulinzi, Petr Cech  amemuweka langoni kwa kuwa zama za Mourinho msimu wa 2004-05 aliruhusu jumla ya mabao 15.


Javier Zanetti naye pia ameunganishwa kwenye kikosi hicho alifanya kazi na  Mourinho ndani ya  Inter Milan na walishinda mara mbili taji la  Serie A,  Claude Makelele amemuweka upande wa kiungo na  Frank Lampard ambaye kwa sasa ni Kocha Mkuu wa Chelsea amejumuishwa kwenye kikosi hicho pamoja Mesut Ozil ambaye alifanya naye kazi ndani Real Madrid ilipoweka rekodi ya kufikisha jumla ya pointi 100.

Eden Hazard pia amejumuishwa kwenye kikosi hicho na mshambuliaji wake ni Cristiano Ronaldo raia wa Ureno na wa mwisho ni raia wa Ivory Coast Didier Drogba mwili jumba fahari ya Afrika.

Ibrahimovic alifanya kazi na Mourinho ndani ya Inter Milan na Manchester United, pia Pogba alifanya naye kazi ndani ya United ila hakuwa na furaha chini ya raia huyo wa Ureno.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic