November 13, 2020

 


IMEELEZWA kuwa uongozi wa Simba umemalizana na kiungo Clatous Chama kwa kumpa dili la miaka miwili kutokana na kuhitaji huduma ya nyota huyo ambaye anatajwa kuingia kwenye rada za watani zao wa jadi Yanga.


Chama mwenye tuzo ya mchezaji bora kwa msimu wa 2019/20 baada ya kufunga mabao mawili na kutoa jumla ya pasi 10 amekuwa bora pia kwa msimu wa 2020/21 ambapo ametoa jumla ya pasi tano na kufunga mabao mawili jambo ambalo limewafanya Yanga kuingia kwenye hesabu za kuitaka saini yake.


Kumekuwa na mvutano mkubwa kuhusu ishu ya Chama kumalizana na Simba kwa kuwa awali habari zilieleza kuwa dau ambalo Simba waliweka mezani ilikuwa ni milioni 150 na Yanga wakaweka dau la milioni 300 kupata saini yake.


Kutokana na dau hilo la Yanga kuwa kubwa limewafanya mabosi wa Simba kuvunja 'benki' kupata saini yake.


"Ule mvutano sasa umekwisha kwani mabosi wa Simba wamekubali kuongeza mkwanja na kumpa dili la miaka miwili hivyo Yanga hawataweza kumpata," ilieleza taarifa hiyo.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa hakuna mchezaji wa timu hiyo anayeweza kuondoka ikiwa atakuwa kwenye mpango wa timu.


"Hakuna mchezaji ambaye anaweza kuondoka ikiwa atakuwa kwenye mpango wa timu na tunamhitaji, unapomzungumzia Chama (Clatous) ni mchezaji mkubwa na uwezo wake unajulikana.


"Kusema kwamba aende upande wa pili sijui itakuaje lakini hakuna kitu kama hicho," amesema.


Injinia Hersi Said, Mkurugenzi wa Kampuni ya GSM ambao ni wadhamini wa Yanga ameweka bayana kuwa wanaheshimu mkataba wa Chama, (Clatous) ila ikitokea watamhitaji mchezaji atakayependekezwa na kocha hawatashindwa kumpata.


Chama jana alikuwa kwenye majukumu ya timu yake ya Taifa ya Zambia ambapo ilikuwa na mchezo dhidi ya Botswana kwa ajili ya kufuzu Afcon na ilishinda kwa mabao 2-1 Uwanja wa Mashujaa.



2 COMMENTS:

  1. Dili la chama liliisha siku nyingi kwa dau la mil 200,watu walibeza lakini tunaanza kuelewana polepole,simba haiwezi kuvunja bank kwa mil 200.

    ReplyDelete
  2. Mshaongea sana kuhusu chama lkn mkaishia kuchutama kwa mnyama.Utopolo bdo njaa ipo unawasumbua.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic