November 13, 2020


 SIMON Msuva, winga wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa wachezaji wamekubaliana kupambana leo kupata matokeo chanya kwenye mchezo wa kuwania kufuzu Afcon 2021.


Hii inakuwa ni mechi ya tatu kwa Stars iakayochezwa Uwanja wa Olympique de Rades nchini Tunisia na mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Novemba 17, Uwanja wa Mkapa.

Mchezo wa leo Novemba 13 ugenini unatarajiwa kuchezwa majira ya saa 4:00 ikiwa kundi J na timu nyingine ni Libya na Guinea ya Ikweta.


Nyota watatu watakosekana ambao ni Thomas Ulimwengu na Adam Adam ambao hawa niwashambuliaji walipata matatizo kwenye suala la kupata hati za kusafiria na Mbwana Samatta ambaye ni nahodha yeye ni ameshauriwa na madaktari kukaa nje ya uwanja kwa muda wa siku 10.


Msuva amesema :"Kazi ni kubwa na kila mmoja anatambua kwamba tunakwenda kwenye ushindani ila kinachotakiwa kwa sasa ni kuungana kwa pamoja na Watazania waendelee kutuombea dua.


"Wapinzani wetu wapo vizuri hilo tunalijua kwa kuwa wamecheza mechi zao mbili bila kupoteza ila hilo halitupi tabu nasi pia tunahitaji ushindi,".


Kikosi hicho jana kilifanya mazoezi ya mwisho nchini Tunisia kwa ajili ya kusaka pointi tatu muhimu. Kikiwa kimecheza mechi mbili kilishinda moja na kupoteza moja kibindoni kina pointi tatu.

3 COMMENTS:

  1. Tunaomba wachezaji waondoe tofauti zao na jinsi wanavyozitumikia club zao Basi wajitahidi kutumikia na taifa vzr Ila nasikitika kukosekana hao wachezaji watatu wamgekuwepo ningekuwa kocha ningewaanzaisha wote wacheze pembeni maana Wana Kasi sana

    ReplyDelete
  2. Tunajua mnafungwa siyo chini ya tatu. Ukweli utakuweka guru.

    ReplyDelete
  3. Hati za kusafiria kuwa tatizo ni mambo ya kizama,kwa hali hii ya utandawazi tunazungumzia upuuzi huu.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic