November 29, 2020

 


JAMES Kotei kiungo wa zamani wa Klabu ya Simba anatajwa kuingia kwenye rada za mabosi wake wa zamani kwa ajili ya kupata saini yake kwenye dirisha dogo linalotarajiwa kufunguliwa Desemba 15.

Simba ambao ni wawakilishi wa Tanzania kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika,  leo wana kazi ya kumenyana na Plateau United,  nchini Nigeria kwenye mchezo wa awali.

Habari zinaeleza kuwa Sven Vandenbroeck amewaambia mabosi wake kuwa nyota huyo anaweza kumfaa ikiwa atawakosa wale ambao amewapendekeza hivyo uwezekano wa kurejea Bongo kwa Kotei upo mikononi wa raia huyo wa Ubelgiji. 

Rekodi zinaonyesha kwamba raia huyo wa Ghana ambaye amefanya kazi kwa ukaribu na Jonas Mkude akiwa Simba msimu wa 2016-19 alicheza jumla ya mechi 75 na kufunga  bao moja.

Baada ya kusepa ndani ya Simba aliibukia Kaizer Chief ya Afrika Kusini kisha akasepa mpaka Slavia-Mozŕy.


Kwa sasa Simba ina kazi ya kusaka kiungo mkabaji ili aungane nao kwenye michuano ya kimataifa kwa kuwa kiungo wao mmoja ambaye ni chaguo namba moja la Sven, Gerson Fraga kwa sasa anasumbuliwa na majeraha ya goti na atakuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu.


Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wakati wa usajili watafanya mambo makubwa kwa kuwa wamejipanga vizuri.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic