LEO Novemba 28 Uwanja wa Mkapa, Yanga inayonolewa na Cedric Kaze itakuwa na kibarua cha kumenyana na JKT Tanzania inayoongozwa na Abdalah Mohamed, ‘Bares’ ambaye amekuwa akipata matokeo ya kusuausa ndani ya ligi.
Kaze anaingia uwanjani akiwa na kumbukumbu ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC, anakutana na JKT Tanzania iliyotoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Mbeya City.
Kaze ameweka wazi kuwa alitumia muda wa mwaka mzima kuwafuatilia wapinzani wake JKT Tanzania ambao atakutana nao Uwanja wa Mkapa.
“Ni kwamba sikuwa nchini Tanzania ila nilikuwa nje ya nchi, nilianza kuifuatilia ligi ya hapa kwa muda mrefu zaidi ya mwaka mmoja hivyo timu zote zinazoshiriki ligi ikiwa ni pamoja na Namungo, Simba, JKT Tanzania ninatambua namna falsafa yake ilivyo.
“Sina mashaka ninapoingia ndani ya uwanja na timu kwa kuwa kazi huwa inakuwa ni moja tu kutafuta ushindi hivyo ninawaambia mashabiki wangu neno moja tu waje uwanjani watupe sapoti,” alisema Kaze.
Yanga ni vinara wa ligi wakiwa na pointi 28 baada ya kucheza mechi 12 inakutana na JKT Tanzania iliyo nafasi ya 15 na pointi 10.
Yanga haijapoteza mchezo ndani ya dakika 1,080 inakutana na JKT Tanzania ambayo imetumia dakika 540 ambazo ni mechi sita kuyeyusha pointi tatu ambazo jumla ni pointi 18.
Kwa maneno tu huna tofauti na mwinyi zahera.... Muda utaongea
ReplyDeleteSupport mia mia. Mwaka mzima akiwa amepewa mkataba upi wa kuifundisha tinu ipi hapa Tanzania? Kaze ana majigamnbo yatakayoyeyuka kama barafu siku si nyingi.
Deletesawa mtabiri na mnajimu...dua la kuku halimpati mwewe
Delete