November 28, 2020

 


TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 20,Ngorongoro Heroes inatarajiwa kushuka uwanjani kumenyana na timu ya Taifa ya Sudan Kusini Novemba 30.


Mchezo huo ni wa hatua ya nusu fainali baada ya Ngorongoro Heroes kutinga hatua hiyo kwa kushinda mechi zake zote mbili kwa ushindi wa mabao mengi.


Mchezo wa kwanza Ngorongoro Heroes ilishinda mabao 6-1 dhidi ya Djibouti na mchezo wa pili ilishinda mabao 8-1 dhidi ya Somalia na mechi zote zilichezwa Uwanja wa Black Rhino, Karatu Arusha.


Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Jamhuri Kihwelo, 'Julio' imekuwa na safu imara ya ulinzi kwenye mechi zake za mwanzo hivyo ina kazi ya kufanya kwenye hatua ya nusu fainali ili kuweza kutinga fainali na kutwaa taji hilo.


Akizungumza na Saleh Jembe, Julio amesema kuwa wachezaji wapo tayari kwa ajili ya ushindani na watapambana kufikia malengo ya kutwaa taji hilo.


"Kila mchezaji anatambua kwamba tupo kwenye ushindani na kinachotakiwa kwa sasa ni ushindi hivyo maandalizi yetu yanaendelea na mashabiki waendelee kutupatia sapoti," amesema.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic