November 8, 2020

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa wachezaji wake jana Novemba 7 walionyesha bidii kwenye kuska matokeo kipindi cha kwanza ila mambo yalibadilika kipindi cha pili na kuwa magumu kwetu.


Yanga ilianza kufunga bao la kwanza kupitia kwa Michael Sarpong dakika ya 31 kwa mkwaju wa penalti ikiwa ni bao lake la kwanza ndani ya Yanga kwenye mchezo wake wa dabi na bao lake la tatu jumla.


Kwa upande wa Simba, Joash Onyango ambaye ni beki yeye alisababisha penalti hiyo dakika ya 30 kwa kumchezea faulo Tuisila Kisinda kisha aliweza kusawazisha bao dakika ya 86 kwa kichwa akimalizia kona ya kiungo Luis Miquissone.


Kaze amesema:"Wachezaji walicheza vizuri kipindi cha kwanza ila kipindi cha pili mambo yalikuwa magumu kwa upande wao jambo ambalo liiwafanya waruhusu bao.


"Unajua tulikuwa tunacheza na timu ambayo ina muunganiko kwa muda mrefu jambo ambalo niliwaambia wanapaswa kuwa makini ila kwa walichokifanya ninawapa pongezi."


Yanga ipo nafasi ya pili ikiwa imecheza mechi 10 na kibindoni ina pointi 24 kinara ni Azam FC mwenye pointi 25, Simba nafasi ya tatu na pointi zake ni 20.

15 COMMENTS:

  1. Kocha anaendelea kukiri Yanga haina muunganiko. Dah! Sasa timu itapata lini muunganiko inaelekea itachukua muda mrefu kwa wachezaji hawa classic kabisa walioigharimu GSM billioni 2.5 kutengeneza muunganiko wa kikosi. Au kocha abadilishwe tena?

    ReplyDelete
    Replies
    1. Kupata muunganiko wa timu sio kazi ya wiki moja au mwezi mmoja. Ni suala la muda mrefu. Utafananisha muda ambao wachezaji wa mikia FC wameshakuwa pamoja na wale wa Yanga SC???

      Delete
  2. Ile haikuwa peneti halali Kwasabsbu ilionesha wazi Kuwa faulo ilifanyika nje ya mstari

    ReplyDelete
    Replies
    1. Ni kama ile ya Kagere vs Yondani,Jitahidini muwe mna tunza kumbukumbu vizuri...

      Delete
    2. Ni kama ile ya Kagere vs Yondani,Jitahidini muwe mna tunza kumbukumbu vizuri...

      Delete
    3. Waelezee hao mikia FC kuwa malipo ni hapa hapa duniani. What goes around, comes around. Wawe wanaandika kwenye diaries zao (kama wanazo)

      Delete
  3. Kipindi cha pili timu ilipotea hasa baada ya Lamine kutoka.

    ReplyDelete
  4. Kipindi cha pili timu ilipotea hasa baada ya Lamine kutoka.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Nakubaliana nawe ndugu, hata baada ya Sarpong kutolewa, mabeki wa mikia FC wakarelax kabisa na kuanza kupanda mbele

      Delete
    2. Sasa kwa nini Sarpong alitolewa? Kama alikuwa bora, kwa nini aingizwe Yacouba?

      Delete
  5. Kweli kabisa Churaaa fc aka krooo krooo krooo walizidiwa sana simba wangewewea kufunga hata goli mbili

    ReplyDelete
  6. Fact.baada ya kisinda kujirusha ndani ya boksi na onyango akajirusha Kwenye boksi.why?alianza kumlalia nje ya boksi.lkn mpaka wanagusa mstari kichwa cha beki kinagusa miguu.labda tumlazimishe refa muda wa kupiga filimbi.

    ReplyDelete
  7. Matefa sita maamuzi sifuri. Wanaongeza gharama kuhonga kwa ile timu iliyotangaza kuupata ubingwa kupitia kwa mfadhili na sio kwa wachezaji na benchi la ufundi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Marefa wetu hawaomi aibu!. Marefu wa Kenya wanaaminiwa hadi wanachezesha mechi kubwa za bara la Afrika. Kuna mechi ya kimataifa ya Simba katikati alisimama refa kijana mdogo kabisa Mkenya. Marefa wetu hawakuona hata ule wivu wa maendeleo?

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic