November 8, 2020


 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kupata sare ya kufungana baoa 1-1 dhidi ya Yanga jana Novemba 7 haikuwa kwenye mpango wake wa kazi.


Simba wakiwa ugenini walikubali kugawana pointi mojamoja na watani zao wa jadi Yanga ambao walikuwa ni wenyeji kwenye mchezo huo.

Michael Sarpong alianza kupeleka maumivu kwa Simba dakika ya 31 kwa mkwaju wa penalti na Joash Onyango aliweka mzani sawa dakika ya 86.


Sven mwenye kibarua cha kutetea taji la Ligi Kuu Bara amesema kuwa ilikuwa ngumu kuamini kwamba ameambulia sare kutokana na maandalizi waliyofanya.


"Tulikuwa na maandalizi mazuri licha ya kwamba tuliwakosa wachezaji wetu wengine ikiwa ni pamoja na Meddie Kagere na Chris Mugalu.


"Yote ambayo yametokea tunayachukua na tutayafanyia kazi kwa ajili ya mechi zijazo, haikuwa mpango wetu kuambulia sare tulikuwa tunahitaji ushindi," amesema.


Simba ipo nafasi ya tatu ikiwa na pointi 20 inaachwa na Yanga kwa pointi nne kwa kuwa imefikisha pointi 24 ikiwa nafasi ya pili zote zimecheza mechi 10 na kinara ni Azam FC mwenye pointi 25.

5 COMMENTS:

  1. Yupo sahihi kabisa kwani ile ilikuwa Simba VS Refs not Yanga.

    ReplyDelete
  2. Kwa nilichokiona jana ni kama Yanga wamezionesha timu zingine madhaifu ya Simba tutarajie maumivu zaidi toka kwa "timu ndogo" zilizoko ligi kuu na pia Simba wabadilike kama wanataka matokeo mechi za kimataifa. Vinginevyo maumivu makali yaja.

    ReplyDelete
  3. Hakuamipongoyenu droo kwaio yanga ilikua mipongo yaodroo misukule nyiemumezoea kubebwa inafika wakati marefali hatawakilazimishwa na tff yenu wanachoka

    ReplyDelete
  4. Kwahiyo nani alishakiri kuwa yeye ni mwizi au ni mchawi mbele za watu! Kiufupi tu SIMBA mliponea kwenye tundu la sindano na kifo kiliwatapika tu ila mlitakiwa kufa mapema, MISUKULE fc ni timu ya kawaida sana, laiti kama lamine moro angekuwepo mpaka mgeomba pooo nguruwe fc nyie

    ReplyDelete
  5. Yanga waache kucheza kutumia marefa, ni aibu maana ubaya ni kuwa football ni mchezo wa hadharani, sio kama kupiga kura na kusubiri matokeo nyumbani

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic