TIMU ya Kenya leo Novemba 27 imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sudan kwenye mchezo wa mashindano ya Cecafa kwa wachezaji wa timu za Taifa chini ya miaka 20.
Kenya na Sudan ambazo zipo kundi C zilishuka uwanjani leo kusaka pointi tatu muhimu kwenye mashindano hayo ambayo Tanzania ni wenyeji.
Mabao ya Kenya yalifungwa na Fortune Omolo dk ya 58 na Benson Ochieng dk ya 90.
Kwa upande wa Sudan walipata bao la kufuta machozi dk ya 85 kupitia kwa Al Gozoli Nooh, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Arusha.
Ushindi huo kwa Kenya unaipa nafasi ya kutinga hatua ya nusu fainali baada ya kufikisha pointi sita sawa na Tanzania ambayo ipo kundi A.
0 COMMENTS:
Post a Comment