BONDIA wa ngumi za kulipwa nchini, Idd Pialali, kesho Jumamosi Novemba 28 anakibarua kigumu mbele ya mkali kutoka Ufilipino, Arnel Tinampay katika pambano lisilokuwa la ubingwa ambalo litapigwa kwa raundi nane katika Ukumbi wa Next Door Arena uliopo Masaki jijini Dar.
Mbali ya Pialali, Mtanzania mwengine, Salim Mtango kutoka mkoani Tanga anacheza pambano la ubingwa UBO kwa raundi 12 dhidi ya Eduardo Mancito kutoka Ufilipino chini ya udhamini wa Gazeti la Spoti Xtra, +255 Global Radio, DSTV, Smart Gin, Plus Tv, Clouds Media, Kebbys Hotel, Uhuru FM na Precision Air.
Mabondia hao leo Novemba 27 walipima uzito katika Uwanja wa Las Vegas uliopo Mabibo jijini Dar ambapo kila mmoja aliweza kutambia kuwa atamkalisha huku kivutio kikubwa kilikuwa mabondia wengi kuja na magari ya maana akiwemo Ramadhani Shauri kutinga uwanjani hapo akiwa ndani ya Hummer.
Pialali baada ya kupima amesema: “Tinampay amekayanyaga nyaya, nataka kuwaonyesha Watanzania wenzangu namna nitakavyomchapa pale ndani ya Next Door, hatovuka raundi tatu, nimejipanga kumaliza utata kabisa.”
Kwa upande wa Tinampay amesema kuwa:- “Sina muda wa kuongea sana lakini naamini nitamchapa mapema mpinzani wangu kwa kuwa tayari ameshaingia uwoga wa kupigana baada ya kuchelewa kufika kupima uzito, njooni kwa wingi muone wenyewe.”
Mabondia wengine watakaopigana leo ni Seleman Kidunda dhidi ya Said Mbelwa watakaopigania mkanda wa ubingwa wa PST, Adam kipenga na Adamu Yusuph nao watapigania ubingwa wa PST wakati Lulu Kayage na Stumaini Muki watamaliza ubishi.
Japhet Kaseba yeye atakuwa na kazi moja na Iman Mapambano, Ramadhan Shauri akitarajia kucheza dhidi ya Salehe Mkalekwa, Ismail Galiatano kutoka pia JWTZ atazichapa na Mustafa Doto, wakati Hajat Shomari akitarajia kumalizana na Leilah Yazidu.
Kwa upande wa tiketi za pambano hilo zinauzwa kwa Sh 20,000 mzunguko, Sh 50,000 kawaida na Sh 100,000 kwa VIP huku zikipatikana kupitia Nilipe App, maduka ya Vunja Bei Store na Vunja Bei Toto Sinza, Shishi Food (Kinondoni), pia Cake City ya Salasala.
Sehemu nyengine ambazo tiketi zitakuwa ni Kaites Lounge ambayo inapatikana Tabata na Dickson Sound ya Magomeni.
0 COMMENTS:
Post a Comment