November 26, 2020


 THADEO Lwanga, kiungo anayecheza soka la kulipwa nchini Misri ndani ya Klabu ya Tanta anatajwa kuingia kwenye rada za Simba.


Lwanga ambaye ameletwa duniani Mei 21, 1994 ana umri wa miaka 26 ni raia wa Uganda.


Kwa sasa anakipiga ndani ya Klabu ya Tanta alijiunga nayo akitokea Klabu ya Vipers aliyoitumika msimu wa 2017-19 akitokea Klabu ya SC Villa.

Mafanikio yake ndani ya SC Villa alicheza jumla ya mechi 50 na kutupia mabao nane.

Imeelezwa kuwa Simba ipo katika hesabu za kupata saini ya kiungo mkabaji huyo kama mbadala wa raia wa Brazil Gerson Fraga ambaye yupo nje ya uwanja msimu mzima kwa majeruhi.

Fraga alipata majeruhi hayo alipokuwa kwenye majukumu yake ndani ya Uwanja wa Mkapa wakati Simba ikipambana na Biashara United na ilishinda mabao 4-0.

2 COMMENTS:

  1. Simba tusifanye maigizo kwenye usajili wa dirisha Dogo hasa kwenye nafasi hii ya kiungo mkabaji.Nafasi ya Kiubgo mkabaji ndio iliotugharimu kwenye champion league mbili zilizopita na kwa mimi binafsi nnaamini nafasi hiyo ya kiungo mkabaji ndio itakayotugharimu kutokufikia malengo kwenye champion league hii pia na tusipokuwa makini itatugharimu kwenye Ligi kuu pia. Kuna fitina nyingi zinaendelea nje ya uwanja za kutudhoofisha simba zinazolengwa moja kwa moja kwa wachezaji wetu kabla ya mechi husika. Na simba tusipokuwa makini basi tutavurugika mapema kwenye mipango yetu ya ubingwa wa ligi na caf champion league.Utopolo wanajaribu to walk toe to toe with us.sometime it lookalike they over pause us especial on past signing and pre preparation match tactics. Simba nguvu kubwa wananchi hawapaswi kuja kutuchezea sharubu kama vile wanacheza na paka wa bibi.

    ReplyDelete
    Replies
    1. sio lazima uandike kwa kiingereza. kama hukikui achana nacho

      Delete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic