UONGOZI wa KMC umesema kuwa mchezo wao dhidi ya Azam FC utakuwa na ushindani mkubwa ila wamejipanga kupata pointi tatu.
KMC ipo nafasi ya 6 imefunga jumla ya mabao 14 na pointi zake ni 15 inakutana na Azam FC iliyo nafasi ya kwanza na pointi 25 huku ikiwa imefunga mabao 18.
Novemba 21 zitakutana Uwanja wa Uhuru kusaka pointi tatu saa 10:00 jioni.
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa KMC, Christina Mwagala amesema kuwa wachezaji wapo tayari na maandalizi yapo sawa.
"Kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wanatambua kwamba kazi itakuwa ngumu kusaka pointi tatu lakini tupo tayari.
"Mashabiki wajitokeze kutupa sapoti kwa kuwa tunaamini kwamba uwepo wao ndani ya uwanja ni mwanzo wetu wa kupata ushindi," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment