NYOTA wa Kabu ya Biashara United, Abdulmajid Mangalo ambaye pia ni nahodha wa timu hiyo anatajwa kuingia anga za Simba.
Mangalo ambaye ni kiraka mwenye uwezo mkubwa wa kucheza nafasi ya beki wa pembeni inaelezwa kuwa mabosi wa Simba wamevutiwa na uwezo wake wanahitaji kumoongeza kwenye kikosi hicho ambacho kinashiriki Ligi ya Mabingwa Afrika.
Habari zinaeleza kuwa sababu ya Mangalo kupewa dili hilo ni kuweza kumpa sapoti beki wao mahiri Shomari Kapombe ambaye anasaidiana na David Kameta,'Duchu' ambaye yupo Arusha na timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20.
"Mangalo ni miongoni mwa wachezaji ambao wanahitajika ndani ya Simba ikiwa mambo yatakwenda sawa ili kuongeza nguvu hasa kwa upande wa beki wa pembeni ambapo anacheza yule Kapombe," ilieleza taarifa hiyo.
Kapombe amekuwa ni chaguo la kwanza kwa Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck kwenye mechi zote 10 amekuwa akianza kikosi cha kwanza jambo ambalo limemfanya kocha apambane kumpata mtu mwingine atakayempa changamoto.
Source of information?
ReplyDelete