November 2, 2020


 BAADA ya Oktoba 31 Simba kuifunga kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Mwadui FC ndani ya Novemba ina kazi ya kusaka pointi 15 kwa kuwa itamenyana na timu tano ndani ya uwanja. 

Kazi kubwa itakuwa ni kusaka pointi sita ikiwa nyumbani mbele ya Kagera Sugar na KMC.


Pointi tisa itasaka ikiwa ugenini ambapo ni mbele ya Yanga, Coastal Union na Dodoma Jiji.


Ratiba yake ipo namna hii:-Novemba 4 itaikaribisha Kagera Sugar, Uwanja wa Uhuru.


Novemba 7 itakaribishwa na Yanga, Uwanja wa Mkapa.

Novemba 21 itakutana na Coastal Union, Mkwakwani.


Novemba 24 itakuwa na kazi mbele ya Dodoma Jiji Uwanja wa Jamhuri na itafunga kazi na KMC Uwanja wa Uhuru, Novemba 29.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic