November 9, 2020


 KOCHA Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa kuumia kwa beki wake kisiki Lamine Moro kulivuruga hesabu zake na kufanya umakini kwa safu ya ulinzi kupungua jambo ambalo liliruhusu bao la usawa kwa wapinzani wake Simba.


Moro raia wa Ghana aliwahi kufanya majaribio ndani ya kikosi cha Simba zama za Kocha Mkuu, Patrick Aussems maarufu kama uchebe ila hakupewa nafasi kwa kuwa tayari beki kisiki Pascal Wawa alikuwa kwenye ubora wake ndani ya kikosi hicho.


Yupo zake ndani ya Yanga akifanya kazi kwa ukaribu na beki mzawa, Bakari Mwamnyeto ambaye jina lake lipo kwenye orodha ya wachezaji 27 wa timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars iliyopo Instanbul kwa sasa kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kuwania kufuzu Afcon dhidi ya Tunisia utakaochezwa Novemba 13, Uwanja wa Mkapa.


Kaze amesema kutoka kwa Moro kipindi cha pili wakati Yanga ikiiongoza bao moja lililofungwa na Michael Sarpong kuliwapa nafasi Simba kuongeza mashambulizi kwa kuwa awali mshambuliaji John Bocco aliwekwa chini ya ulinzi na beki huyo.

"Tulikuwa na mpango mmoja wa kuzuia na kushambulia, alipoumia Moro hapo mpango namba moja ukafeli wa kulinda chaguo likawa kwenye kushambulia zaidi.


"Ila sio mbaya naona Makapu,(Said) alifanya kazi yake kwa umakini na anaonyesha bidii kwa wakati ujao tutakuwa tumejifunza jambo la kufanya kwani maisha lazima yaendelee," .

Bao la Simba iliyo nafasi ya pili na pointi 20 lilifungwa na Joash Onyango dakika 4 kabla ya mpira kumalizika.

Yanga ikiwa imecheza mechi 10 haijapoteza mchezo na safu yake ya ulinzi imeruhusu mabao matatu ya kufungwa na ile ya Mwadui FC inashika namba moja kwa kuruhusu mabao mengi ambayo ni 20.

3 COMMENTS:

  1. Simba inashika nafasi ya pili kwenye ligi ya muungano au kagame cup????

    ReplyDelete
  2. heeh heeh heeh........mapinduzi cup.

    ReplyDelete
  3. Hiyo ndiyo mzee wa kutunga story

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic