KOCHA Mkuu wa Yanga, Mrundi, Cedric Kaze, amewaambia vijana wake kuwa, katika mchezo wa kesho Jumamosi dhidi ya Simba, anataka bao ndani ya dakika 20 kipindi cha kwanza kwa lengo la kuwaondoa mchezoni wapinzani wao hao.
Simba na Yanga zinatarajiwa kuvaana kwenye Uwanja wa Mkapa jijini Dar ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.
Katika kuelekea mchezo huo, Jumatano usiku kikosi cha Yanga kilirejea jijini Dar kikitokea Mwanza baada ya kucheza na Gwambina na mchezo huo ulikamilika kwa sare ya bila kufungana na moja kwa moja kikaingia kambini kwenye Kijiji cha Avic Town, Kigamboni, Dar.
Akizungumza na Spoti Xtra, Kaze alisema kuwa anazipenda mechi za dabi hivyo hana hofu, kikubwa ameandaa mipango mikakati kwa wachezaji ili kuhakikisha anapata ushindi wa mapema katika mchezo huo.
“Malengo yangu ni kuimaliza dabi kwa kupata ushindi wa mapema na kufunga dakika za mwanzo hadi kufikia dakika ya 20, hilo linawezekana kwetu, kwani maandalizi niliyoyafanya yanatosha kupata ushindi.
"Siyo mchezo mwepesi kwani wapinzani wetu nao wamejiandaa vizuri, lakini kama kocha nimepanga kuingia kitofauti katika mchezo huo.
“Mchezo huo unahitaji mbinu, akili na ufundi mwingi ili kuwazidi wapinzani wetu, kikubwa niahidi kucheza mchezo mzuri wa kuvutia kwani uwanja tutakaoutumia ni mzuri tofauti na ule tuliocheza dhidi ya Gwambina,” alisema Kaze.
Hayayetu macho
ReplyDeleteYanga mwaka huu ni sawa na mwaka juzi wakati wa Zahera ilikuwa ikishinda hivyo hivyo bao moja au mbili moja na ushindi wenyewe unapatikana kuanzia dakika ya 70.Mwaka juzi walikuja ondolewa kwenye uongozi wa ligi zikiwa zimebaki mechi sita. Sasa kama wamekuwa wakishinda hilo bao moja kuanzia dak ya 70 ni kwa Simba ndiyo watalipata dak ya 20?..Kiuhalisia hamna tofauti ya matokeo Yanga kati ya huyu kocha na aliyetoka kutimuliwa..huo ndiyo ukweli
ReplyDelete