November 6, 2020

 


OBREY Chirwa, mshambuliaji ndani ya kikosi cha Azam FC kwa sasa yupo fiti kuendelea na mapambano ndani ya timu hiyo baada ya kupata majeraha kwenye Oktoba 20 wakati timu yake ikisepa na pointi tatu dhidi ya Ihefu kwenye ushindi wa mabao 2-0.


Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Sokoine, wazawa wawili walitupia mabao kwenye mchezo huo ambao ni Idd Seleman na Lyanga.

Azam FC ni vinara kwenye ligi wakiwa na pointi 25, imeweza kupata ushindi wa mabao 18, ambapo katika mabao hayo, Chirwa amefunga mabao manne na kutoa asisti mbili katika michezo yote aliyocheza kabla ya kuuguza jeraha.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria amesema kuwa tayari Chirwa yupo fiti baada ya kupata majeraha ya kifundo cha mguu.

“Chirwa amerudi na amekwisha maliza mazoezi ya viungo baada ya kusumbuliwa na jeraha alilopata kwenye mchezo dhidi ya Ihefu uliochezwa Uwanja wa Sokoine.

“Kwa sasa, ameweza kurudi katika hali yake ya uimara, tayari kwa mashambulizi katika kikosi yatakayoifanya Azam FC ipate ubingwa msimu huu wa 2020/21 kwenye Ligi Kuu Bara,” amesema Zakaria.


 Mshambuliaji huyo alikosekana kwenye mechi mbili, ambazo ni Azam dhidi Mtibwa Sugar Oktoba 26 Uwanja wa Jamhuri, ambapo Mtibwa ilipata ushindi wa 1-0 na Azam dhidi ya JKT Tanzania Oktoba 30 katika Uwanja wa Azam Complex ambapo wote walitoka sare ya 1-1. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic