November 28, 2020


 MABINGWA wa kihistoria wa Ligi ya Mabingwa Afrika, Al-Ahly ya Misri,  jana usiku Novemba 27 wamefanikiwa kutwaa ubingwa wa tisa baada ya ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya mahasimu wa Zamalek.

 

Zamalek ambao hawajatwaa ubingwa tangu walipovuliwa na Simba mwaka 2003, walikuwa wa kwanza kupata bao kupitia kwa Suyala dakika ya 5, Al-Ahly walisawazisha bao hilo dakika ya 39 likifungwa na Shikabala.

 

Wakati wengi wakiamini kuwa mechi hiyo ya ‘Cairo Derby’ watashuhudia dakika 120, mchezaji wa Al-Ahly, Ashfa, aliweka kambani goli la dakika ya 88 ambalo liliwahakikishia ubingwa.

 

Kocha wa Al Ahly ya Misri, Pitso Mosimane, ametwaa taji lake la pili la klabu Bingwa Afrika baada ya kufanya hivyo kwa mara ya kwanza 2015/2016 akiwa na Mamelodi Sundowns ya kwao Afrika Kusini.


Baada ya kuiwezesha Al Ahly kutwaa taji la tisa la Ligi ya Mabingwa Afrika kutokana na kukaa na ukame kwa miaka saba, inaarifiwa kuwa Pitso atapewa bonasi ya dola za Marekani 500,000 (Tsh Bilioni 1.1).

 

Pitso anaingia katika rekodi ya kuwa kocha wa tatu aliyewahi kutwaa mataji ya Ligi ya Mabingwa Afrika mara mbili akiwa na timu mbili tofauti.

1 COMMENTS:

  1. Kua Makin kaka waloanza kupata bao ni Al Ahly na sio zamalek.kama ulivyoripot

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic