November 28, 2020

 


UPO uwezekano mkubwa wa Simba kumtoa kwa mkopo mshambuliaji wake mpya Charles Ilanfya kwenye usajili wa dirisha dogo litakalofunguliwa Desemba 15, mwaka huu baada ya yeye mwenyewe kuomba aondoke.

 

Ilanfya ni kati ya wachezaji wapya waliosajiliwa na Simba msimu huu katika kukiongezea nguvu kikosi hicho kinachojiandaa na mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.


Kwa sasa kipo nchini Nigeria ila Ilanfya ni miongoni mwa wachezaji ambao wameachwa Bongo.

 

Mshambuliaji huyo aliyetokea KMC anawania namba na John Boco, Meddie Kagere na Chris Mugalu, awali alikuwa anawaniwa na Yanga kabla ya kutua Simba kwa dau la Sh Mil 30Mil akisaini mkataba wa miaka miwili.

 

Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, mshambuliaji huyo ameomba kurudi KMC kwa mkopo baada ya kuona hana nafasi katika kikosi cha kwanza chini ya Kocha Mkuu, Mbelgiji, Sven Vandenbroeck.


“Ilanfya alishawahi kuondolewa kambini na kocha Sven kwa kile alichodai kutomuelewa kabisa, hiyo ni baada ya kucheza bila ya kufuata maelekezo yake ambayo amekuwa akimpa akiwa kwenye mechi.

 

“Hiyo ilishawihi kutokea kwa aliyekuwa kiungo wetu (Sharaf) Shiboub ambaye alikuwa hachezi kwa kufuata maelekezo yake ambayo amekuwa akimpa na kusababisha kumuondoa kwenye mipango yake kabla ya kumuachia aondoke zake baada ya mkataba wake kumalizika.

 

“Naye Ilanfya huenda akaondoka Simba kwa kupelekwa KMC kwa mkopo sehemu alipoomba apelekwe. Aliondolewa kwa makusudi kwenye msafara wa kikosi chetu kilichosafiri kwenda Nigeria kucheza na Plateau,” alisema mtoa taarifa huyo.

 

Alipotafutwa Katibu Mkuu wa Simba, Arnold Kashembe kuzungumzia hilo, alisema: “Suala la usajili lipo kwa kocha kwani yeye ndiye anayeamua mchezaji yupi tumsajili na yupi tumuache.”

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic