KIPA namba moja wa Klabu ya Barcelona Marc- Andre ter Stegen, ameanza mazoezi na kikosi hicho baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.
Ter Stegen alitupwa nje baada ya kuumia kwenye
Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu uliopita baada
ya kipigo cha mabao 8-2 dhidi ya Bayern Munich.
Kipa huyo ameanza mazoezi ndani ya kikosi cha timu hiyo, siku ya Alhamisi ya wiki hii
baada ya kuwa nje kwa muda mrefu.
Kwa sasa Barcelona wanamtumia Neto kama kipa
namba moja ndani ya kikosi hicho badala ya Ter Stegen.
Hata hivyo, Barcelona pia ilithibitisha kuwa beki wake Samuel Umtiti pia amepona na sasa yupo kikosini akifanya mazoezi na kikosi hicho kwa sasa.
0 COMMENTS:
Post a Comment