November 2, 2020


 KIUNGO wa kati wa Manchester United, Paul Pogba, amekubali kupokea lawama baada ya kucheza rafu dhidi ya mchezaji wa Arsenal, iliyosababisha penati ambayo iliamua matokeo ya mchezo huo wa ligi kuu ya England.

 

Pogba alinyanyua mguu uliomuangusha Hector Bellerin ndani ya eneo la hatari na Pierre-Emerick Aubameyang akafunga bao lililoipa ushindi Uwanja wa Old Trafford.

 

”Tunajua kwamba kilikuwa ni kiwango duni, mimi binafsi sikupaswa kucheza rafu ya aina ile. Nilidhani ningeugusa mpira lakini sikufanya hivyo. Sikupaswa kutoa adhabu mbaya kama hiyo.




"Nilicheza faulo ya kijinga na nimefanya kosa la kijinga ambalo limeigharimu timu yangu, nimefanya makosa ila hamna namna kwa kuwa nilikuwa ninapambana kutimiza majukumu yangu," amesema Pogba.



0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic