November 28, 2020


 
MKOA wa Ruvuma kwa mwaka 2020 utakuwa ni mwenyeji katika Semina ya mafunzo ya mchezo wa Karate Tanzania, (GASSHUKU 2020).


Semina hiyo inatarajiwa kufanyika kuanza Desemba 4 mpaka Desemba 12 mwaka huu wa 2020 huku maandalizi yakiendelea kwa sasa.

 

 Semina na mafunzo hayo yanayoandaliwa na Shirikisho la mchezo wa Karate Tanzania (JKA/WF-TZ)  yamekuwa yakifanyika katika mikoa mbalimbali kila mwaka na mwaka jana yalifanyika mkoani Morogoro na mwaka huu mkoa wa Ruvuma utakuwa mwenyeji.

 

 Lengo kuu la semina na mafunzo hayo ni kuutangaza mchezo wa Karate Tanzania pamoja na kuangalia viwango vya makarateka nchini Tanzania.

 

Lawrence Mapunda kutoka  kurugenzi ya Idara ya Mahusiano na Habari kwa Umma  ya Shirikisho la mchezo wa Karate Tanzania (JKA/WF-TZ)  amesisitiza kukamilika kwa maandalizi ya GASSHUKU hiyo.


Pia   makarateka watapata fursa ya kufanya mitihani ya mchezo huo itakayosimamiwa na mkufunzi mkuu wa mchezo wa karate Tanzania, Sensei Jerome Mhagama Pamoja na msaidizi wake Mikidadi Kilindo.

 

2 COMMENTS:

  1. Ni wakati gani kucheza Karate inakuwa ugaidi na wakati gani unakuwa mchezo? Kuna baadhi ya misikiti walikuwa wakifanya mazoezi ya karate ikapigwa marufuku huenda Leo tungekuwa na wachezaji wengi wa mchezo huu.

    ReplyDelete
  2. Kalate kalate mna toa ajila xaxa au mna tmiza latba ya kutembeza mwaka jana molo mwaka huu songea

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic