November 28, 2020


WAWAKILISHI wa Tanzania, Simba wapo nchini Nigeria ndani ya mji wa Jos ambapo ndipo makazi ya wapinzani wao Plateau United ambao watakutana nao kesho Novemba 29 kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika huku ikielezwa kuwa wapinzani wao wamekuwa wakiwafanyia michezo ya kuwatoa kwenye mchezo.


Ikiwa chini ya Kocha Mkuu Svend Vandenbroeck, kesho ina kazi ya kusaka ushindi huku ikutana na kibarua kizito cha kupenya mbele ya wapinzani hao ambao wanaonekana kuwa ni watu wenye mipango mingi nje ya uwanja na ndani ya uwanja.


Habari zinaeleza kuwa baada ya kikosi cha Simba kutia timu jana, Novemba 27 mji wa Jos wakitokea Lagos kwenye hotel ambayo walifikia wahudumu waligomea wapishi maalumu wa Simba huku wakitaka watumike wale ambao wapo kwenye hotel zao.


Pia habari nyingine zinaeleza kuwa mbinu ya wapinzani wao ipo kwenye kuwapoteza Simba kwa kuwatoa nyota wake muhimu kwa kutumia vipimo vya Corona ili waukose mchezo huo.


Nyota ambao wanatajwa wapo kwenye hesabu hizo ni pamoja na Clatous Chama, Luis Miquissone, John Bocco na Rarry Bwalya.


Mratibu wa Simba, Abbas Gaza amesema kuwa kwa upande wa maandalizi wamekamilisha kwa asilimia 90 kinachosubiriwa ni masuala ya ndani ya uwanja, ambapo wana imani ya kupata matokeo chanya.

"Kila kitu kinakwenda kwa namna ambavyo kimepangwa, hatuna mashaka tunaamini kwamba yote ambayo yanatokeo huku tutapambana kupata matokeo," .

8 COMMENTS:

  1. Wawaambie kuwa wakipangiwa Corona nao pia watafanyiwa na kufanyiwa kama wanayotaka kuyafanya

    ReplyDelete
  2. Wakifanya hilo wajue wakifika hapa pia tutawapa vipimo fake vya corona wachezaji wai muhimu kama watano hivi

    ReplyDelete
  3. Hawatujui hao kama papai lilikutwa na corona manina zao hadi mipira yao itakutwa na corona

    ReplyDelete
  4. Japokuwa mimi ni shabiki wa Yanga lakini nasema kama ni kweli hawa jamaa wamepanga kufanya uhuni huo wa kutoa majibu feki ya Corona basi wakija huku nao wapewe majibu ya maambukizi ya Corona kuanzia benchi la ufundi,wachezaji hadi vifaa wanavyotumia tukiwa na ushahidi wa papai,sungura na grease kukutwa na corona akati wa majaribio ya vipimo vya maabara maana wanachafua taswira ya nchi yetu

    ReplyDelete
  5. Ubimngwa wa kwao wameupata kwa korona na ubingwa wa afrika wanautaka kwa korona?

    ReplyDelete
  6. Simba mnalo,fungweni tu hukoz mkirudi huku tena kichapo kingine..leo mtani wenu yanga anafikisha point 31 kwenye ligi bila kupigwa.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic