November 6, 2020



IMERIPOTIWA kuwa uongozi wa Klabu ya Manchester United kwa sasa upo tayari kumuuza kiungo wake Paul Pogba raia wa Ufaransa msimu ujao ili akatumike ndani ya Klabu ya Real Madrid inayoshiriki La Liga.


Nyota huyo wa timu ya Taifa ya Ufaransa mwenye miaka 26 amekuwa kwenye kiwango cha chini ndani ya Unted chini ya Kocha Mkuu Ole Gunnar Solksajer ambaye inaelezwa kuwa kwa sasa kibarua chake kipo mashakani kutokana na mwendo mbovu wa timu hiyo.

Pogba alifanya kosa ambalo yeye mwenyewe aliliita ni la kijinga kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Arsenal Uwanja wa Old Trafford na kuifanya timu yake ipoteze kwa kufungwa bao 1-0 na kuyeyusha pointi tatu mazima.

Pia kwenye kikosi cha kwanza hana nafasi jambo ambalo linatoa picha kwamba msimu ujao hatakuwa ndani ya kikosi hicho. Tayari mabosi wa United wameanza kufanya mazungumzo na wale wa Real Madrid inayonolewa na Zinedine Zidane ili kuweza kufika makubaliano ya bei ya kumuuza nyota huyo.

Taarifa zinaeleza kuwa Manchester United wameuliza dau ambalo Real Madrid wanalo ili wamuuze kiungo huyo. Madrid walikuwa na mpango wa kumvuta ndani ya Bernabeu kiungo huyo ila janga la Virusi vya Corona lilitibua mambo na kuwafanya washindwe kufikia makubaliano ya bei.

 

1 COMMENTS:

  1. Wafanye haraka haraka asepe zake maana anatunyima raha.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic