KIUNGO mshambuliaji wa Klabu ya Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy', amefanikiwa kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Azam FC Oktoba, 2020.
Sure Boy ametwaa tuzo hiyo akiwazidi wachezaji wenzake, beki Bruce Kangwa, kiungo mkabaji Ally Niyonzima, washambuliaji Obrey Chirwa na Prince Dube.
Nyota huyo amekabidhiwa tuzo hiyo na Sheikh Twalib, kabla ya kuanza kwa mchezo kati ya Azam FC na Dodoma Jiji uliochezwa jana Novemba 5.
Kwenye mchezo huo Azam FC iliibuka na ushindi wa mabao 3-0 ambayo yanaifanya ipande kileleni kwa kuishusha Yanga nafasi ya kwanza baada ya kufikisha jumla ya pointi 25.
0 COMMENTS:
Post a Comment