TIMU ya Taifa ya Msumbiji inayonolewa na Kocha Mkuu Luis Goncalves ikiwa nyumbani jana ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-0 dhidi ya Cameroon Uwanja wa Estadio do Zimpeto mchezo wa kufuzu Afcon.
Mabao ya Cameroon yalifungwa na Vincent Aboubakari dakika ya 26 na lile la pili lilifungwa na Serge Tabekou dakika ya 73.
Kiungo wa timu hiyo Luis Miquissone ambaye anacheza Klabu ya Simba alisababisha penalti moja dakika ya 20 mpigaji aligongesha mwamba na kuwafanya washindwe kupata bao la mapema.
Ikiwa ipo kundi F, Msumbiji ipo nafasi ya pili na pointi 4 huku vinara wakiwa ni Cameroon ambao tayari wameshafuzu kwa kuwa ni wenyeji wana pointi 10.
Hakuna tatizo nani asiyejua uwezo wa Simba wa Teranga (Cameroon), pia tunaamini Konde Boy hakucheza peke yake na hata hiyo Penalty wala siyo myake ni ya Timu nzima.
ReplyDeleteNilikua naskia anaemiliki hii glop ni utopolo sikuamini ila Leo nimeamini kabisa. Mwandishi acha upumbavu jikite kwenye uandishi acha unazi m*eng* wewe
ReplyDeleteWeeee mbona fara sana....shida nini mpaka umtukane mwandishi......amekulazimisha usome taarifa zake....mitu mingine bhana shida hata kwa wazazi.....mwame mw kashawaambia msiongee chochote yet ndo msemaji ....pumbavu
Delete