November 15, 2020

 




Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji amesema suala la Simba kuwa inamuwania kiungo nyota wa Yanga, Mukoko Tonombe ni propaganda zilizotengenezwa.


Dewji amesema Simba haijawahi kumjadili Mukoko na wala haina habari naye kama inavyoelezwa mitandaoni.



Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dewji amesema kila suala la usajili wa Simba, ni mapendekezo ya kocha.


"Kocha ndiye anependekeza mchezaji gani anatakiwa, huyo mchezaji hatujawahi kumjadili," alisema.


Hata hivyo, Dewji alikiri kuwa Kocha Sven van der Broeek amependekeza kusajiliwa kwa kiungo mkabaji kutokana na Gerson Fraga kuwa majeruhi kwa muda mrefu sasa.


Kutokana na hilo, Dewji aliendelea kusisitiza kwamba suala lao la kumsajili kiungi mkabaji litakuwa ni siri.


"Hiyo ni siri, si kwamba tunazihofia timu za hapa ndani. Lakini tunahofia pia hata zile za nje ya Tanzania kwa kuwa kutokana na mwendo mzuri wa Simba, kumekuwa na ushindani mkubwa sana."


Hivyo karibuni kulizuka taarifa kwamba kutokana na Yanga kuonekana kutaka kumsajili Cleotus Chama kutoka Simba, Msimbazi nao wameamua kuhamishia mashambulizi kwa Mukoko raia wa DRC maarufu kama Ticha.



8 COMMENTS:

  1. Pesa ipo tunaweza kumleta yoyote yule mabingwa wa nchi mara 3

    ReplyDelete
  2. Nilishawaonya ninyi waandishi juu ya kuzushazusha mambo ili mpate habari, mmeona MO anawakana leo? Habari zetu jitahidini zile na uhalisia

    ReplyDelete
  3. Ogopa kusoma habari haina source

    ReplyDelete
  4. Hawa jamaa kwa habari za kutengeneza hawana mshindani

    ReplyDelete
  5. Narudia Tena wachezaji wengi toka utopolo hawana hadhi ya kumchezea mabingwa was nchi, sasa sisi huyo was nn mkiopewa kwa mkopo na as vital.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Utakuwa umelewa wewe siyo bure kwa sababu huna hoja hata moja. Na uwezo wako wa kufafanua hoja na kuzipambanua ni mdogo sana

      Delete
  6. Mo wambye hao wanao toka na malaya wa bas wame sahau ad wake zako na wengne ata mpango wa kuoa hawana

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic