November 15, 2020


 


Kama kuna klabu ina mpango wa kuingia mkataba na kiungo nyota wa Simba, Luis MIquissone, italazimika kusubiri miaka mingine mitatu na nusu au imwage mamilioni mezani pale Msimbazi.


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji amesema mchezaji huyo ana mkataba wa miaka mitatu na nusu na Simba, hivyo hakuna sababu ya kuwa na hofu.


"Kama watahamia kwa Luis, sisi tuko makini sana na tunajua nini tunafanya. Mkataba wake ni miaka mitatu na nusu na hii tunaangalia kwa wachezaji vijana wenye future.


"Sioni kama kuna sababu ya kuwa na hofu, huyu ni mchezaji wetu na vizuri tuendelee na mambo mengine," alisema.


Dewji amejitokeza mbele ya waandishi wa habari leo na kuzungumzia mambo kadhaa yakiwemo yale waliyojadili katika Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, jana.


Mara kadhaa, kumekuwa na taarifa kwa mchezaji huyo raia wa Msumbiji kuwaniwa na watani wao Yanga.


Taarifa hizo zimekuwa zikieleza kwamba Yanga wanamuwania mchezaji huyo kupitia aliyekuwa CEO wa Simba, Senzo Mbatha na aliapa kuwa atatua Jangwani.


Kauli ya Mo Dewji ainafuta taarifa hizo ambazo zimekuwa zikizagazwa mitandaoni kwa makusudi ili kupeleka taharuki.



5 COMMENTS:

  1. Hiyo ni kawaida ya mikundu ya Msimbazi. Inatamani kwa jirani lakini inapoombwa haitoi ushirikiano.

    ReplyDelete
  2. Matusi ya nini sasa!!?? Halafu mkiitwa Mbwa au Manyani mnakasirika

    ReplyDelete
  3. Mikia bhana mbona mnaweweseka........mwemedi kawa msemaji wenu

    ReplyDelete
  4. Kwani Yanga mlimtaka Luis?

    ReplyDelete
  5. Unatia aibu kutukana. Sitaki kuamini wewe na mimi tunashabikia timu moja Yanga.
    Mpira sio ya uadui.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic