November 15, 2020




Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Mohamed Dewji amesema klabu hiyo ilishaingia mkataba mpya na kiungo Cleotus Chama.


Mo Dewji amesema mkataba wao na Chama unaisha mwaka 2022, hivyo taarifa za kuwa anakwenda Yanga zimekuwa zikiwashangaza.


Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Dewji amesema mchezaji huyo ni mali ya Simba na hakuna sababu ya kuwa na hofu.


“Taarifa sijui anakwenda Yanga ni mambo ambayo si sahihi, hakuna sababu ya kuwa na hofu na ninawatoa hofu mashabiki wa Simba kuwa tuko makini sana.


“Sehemu mbalimbali zimekuwa nikikutana na mashabiki wa Simba ambao wananiambia Mo fanya Chama asiondoke Simba. Chama ni mchezaji wa Simba.


“Suala kwamba anakwenda Yanga sijui linatoka wapi lakini haina shida, sasa nimewaambia na ninafikiri leo tunafunga mjadala,” alisema Mo Dewji.



10 COMMENTS:

  1. Hawa viongozi wetu wa Yanga ni lazima sasa waache ujinga na uzushi wao.
    Walizusha wamesaini ba Tshishimbi, wakadwi tuna mkataba na Morisson na sasa Chama. Tunaonekana vioja mitaani.
    Kwamba tunadajili wachezaji hewa.Badilikeni.

    ReplyDelete
  2. Wanasaidiwa na waandishi uchwara ambao walishampangia chama fomesheni tatu tofauti

    ReplyDelete
  3. Utopolo fahamuni kuwa mnaviongozi wasemaji na si watendaji.

    ReplyDelete
  4. Hatubali kuporwa mchezaji wetu Chama. Tutaenda mbele mpaka kieleweke.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Mohamed Dewji amesema kuwa hela zote za usajili yeye anatoa kwa kuwa timu hiyo haina hela.

      Delete
  5. Utopolo tutawakera mpaka basiii, morrisoni kawavuruga mpaka mnaanza kuwehuka. Mpira Ni pesa Kama guns pesa utaishia kubwabwaja tu wenzio wanapeta. Morrisoni kitaambo alitambua utopolo Hamna malengo yanayoeleweka akasepa.

    ReplyDelete
  6. Chama siyo mpumbavu Kama messy na wengine mliowaua viwango na ndoto zao. Ajibu alitambua mapema akasepa kurudi nyumbani. Msahau chama mpaka tumchoke ndo tutawapa maana bado hamjakidhi vigezo vyakuwa naye.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Huyi Ajib alipokuwa Yanga na kwa sasa alivyo kwenu; wapi alikuwa na kiwango bora? Na huyou Kessy hutambui kuwa akiwa Yanga ndipo kukampa nafasi ya kwenda Zambia, na kwa nini alipokuwa kwenu hakuna alichovuna zaidi ya kumkashif amewafungisha kwenye dabi? Mikia wengi hamjitambui

      Delete
  7. Nilimpinga sana mwandishi nikimwambia dili liliisha mapema.Habari zao nyingi zakufikirika.

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic