November 29, 2020

 


STEPHEN Sey, nyota wa Klabu ya Namungo FC amesema kuwa furaha yake ni kuona timu inapata matokeo ndani ya Uwanja jambo ambalo lilimfanya jana Novemba 28 kutupia mabao mawili wakati timu yake ikishinda mabao 3-0 dhidi ya Al Rabita FC ya Sudan Kusini.

Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Azam Complex ulikuwa ni wa hatua ya awali ya Kombe la Shirikisho ambapo kwa Tanzania inawakilishwa na Namungo FC.


Ikiwa ni mara ya kwanza kushiriki michuano ya kimataifa baada ya kupanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2019/20  imeanza kwa ushindi jambo linalotoa matumaini ya kupata nafasi ya kusonga mbele ikiwa wataendelea na spidi ambayo wameanza nayo.


Mabao hayo alipachika kipindi cha kwanza dakika ya 20 na 39 na bao moja lilipachikwa na Shiza Kichuya dakika ya 64.


Sey amesema;"Furaha yangu ni kuona timu inapata matokeo chanya hakuna kingine zaidi ya hilo hivyo tunawashukuru mashabiki kwa sapoti yao wazidi kutupa sapoti, ".


Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Desembe 4-9 nchini Sudan Kusini ambapo Namungo wanahitaji sare ama ushindi wa aina yoyote kusonga mbele.

5 COMMENTS:

  1. Hongereni Saba Namungo mmetutoa kimasomaso watanzania wazalendo. Pamoja tutafika Tanzania hatulali mbele kwa mbele, Simba naamini nanyi hamtituangusha tembezeni kichapo *Simba & Namungo = Tanzania* hivyo Simba na Namungo oyeeee sawa na Tanzania wazalendo oyeeee.

    ReplyDelete
    Replies
    1. Safi sana saf sana namungo kwa ushndi mwenyez mungu awajalie mfike stage group . Ila sasa hao mikia ikiwezekana wapgwe 5 maana siwapendi kama mavi

      Delete
    2. Tangu lini utopolo akawaza maendeleo muda wote anawaza pumba na kuongea utumbo Kama ww kiazi.
      Wanaume Simba ngome isambe kitaifa na kimataifa. Simba nguvu moja

      Delete
  2. safi sna mmeonyesha mlistahili hyo nafac

    ReplyDelete

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic