November 29, 2020


 DEUS Kaseke nyota wa Yanga amesema kuwa anafanya vizuri ndani ya uwanja akianza na Yacouba Songne jambo ambalo linampa furaha yeye pamoja na timu kiujumla.


Kwenye mechi mbili mfululizo ambazo wameanza pamoja jumla wamehusika kwenye mabao mawili na kuipa timu yao pointi sita baada ya kufunga na kupeana  pasi za mwisho.

Mchezo wa kwanza ilikuwa Novemba 25, Uwanja wa Azam Complex wakati Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Azam FC bao la ushindi lilifungwa na Kaseke kwa pasi ya Songne.

Jana Novemba 28, Yanga ilishinda bao 1-0 dhidi ya JKT Tanzania huku bao la ushindi kwa Yanga likifungwa na Kaseke kwa pasi ya Songne na kufanya jumla wakusanye pointi sita na mabao mawili sawa na idadi ya pasi za mwisho ambazo wametengeneza.


Kaseke amesema:"Ninafurahi kucheza na Songne kwa kuwa nimejua aina ya uchezaji wake hivyo tunapambana kwa ajili ya timu na nimeshajua aina ya uchezaji wake," .


Yanga ipo nafasi ya kwanza ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 13, haijapoteza mchezo mpaka sasa na imefungwa mabao manne.

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic