BONDIA namba moja nchini, Hassan Mwakinyo, ametajwa kuwa bondia wa nyota tatu duniani, akihitaji kutafuta nyota nyingine mbili ili kuingia anga za mabondia wanaotamba duniani akiwamo Manny Pacquiao mwenye nyota tano.
Kwa mujibu wa viwango vilivyotolewa na mtandao wa ngumi za kulipwa wa dunia, Boxrec, jana Ijumaa, Mwakinyo amepanda kutoka nafasi ya 78 hadi ya 41 duniani kati ya mabondia 2,050 wa uzani wa super welter.
Bondia huyo licha ya kushinda mapambano kadhaa mwaka huu likiwamo la Tshibangu Kayembe, alibaki nafasi ya 78 mpaka leo vilipotajwa viwango vipya na kupanda hadi nafasi ya 41.
Mwakinyo ameweka wazi mipango yake kwamba ni kuitangaza Tanzania kitaifa na kimataifa kwa kufanya kazi kwa juhudi bila kukata tamaa.
"Malengo yangu makubwa ni kupeperusha bendera ya Tanzania kitaifa na kimataifa, kila siku kwangu ninajifunza na kuongeza juhudi zaidi," amesema.
0 COMMENTS:
Post a Comment