November 28, 2020


 NYOTA wanne leo wanatarajiwa kukosekana kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Yanga na JKT Tanzania unaoatarajiwa kuchezwa Uwanja wa Mkapa kutokana na kusumbuliwa na majeraha.


Yanga chini ya Cedric Kaze ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya JKT Tanzania inayonolewa na Mohamed Abdalah, 'Bares'.


Kwa mujibu wa daktari wa Yanga, Sheck Mgazija ameweka wazi kuwa Shomar Kibwana kwa sasa anaendelea na matibabu baada ya kuumia bega kwenye mchezo dhidi ya Azam FC.


Nyota mwingine ambeye ni majeruhi wa muda mrefu ni Mapinduzi Balama ambaye kwa sasa ameanza mazoezi mepesi.


Kwa upande wa JKT Tanzania, nahodha Mwinyi Kazimoto yeye anasumbuliwa pia na majeraha pamoja na Mohamed Rashid ambaye bado hajwa fiti. 

0 COMMENTS:

Post a Comment

TwitterFacebookGoogle PlusLinkedInRSS FeedEmail

GONGA HAPA KWENDA AZAM TV

B2.jpg
Image and video hosting by TinyPic