UWANJA wa Mkapa, Novemba 28.
FT Yanga 1-0 JKT Tanzania
Yanga inasepa na pointi tatu jumla Uwanja wa Mkapa na kufikisha jumla ya pointi 31.
Zinaongezwa dakika 3
Dakika ya 89 Hassan Twalib wa JKT Tanzania anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea faulo Nchimbi
Dakika ya 88 Mgandila anapiga shuti linalenga nje ya lango
Dakika ya 86 Michael Aidan anaonyeshwa kadi ya njano kwa kumchezea rafu Kisinda
Dakika ya 84 Ditram Nchimbi anaotea
Dakika ya 77 Adam Adam anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 70 Boxer anatoka anaingia Ninja.
Dakika ya 68 Nurdin Mohamed anaonyeshwa kadi ya njano
Dakika ya 67 Kisinda anapewa huduma ya Kwanza,
Dakika ya 66 Boxer anapewa huduma ya kwanza
Dakika ya 58 Adam anafanya jaribio ndani ya 18 halizai matunda
Dakika ya 57 Boxer anafanya jaribio halizai matunda
Dakika ya 54 Fei Toto anatoka anaingia Zawad Mauya, Farid Mussa anaingia anatoka Yacouba Sogne
Dakika ya 54 Kisinda anafanya jaribio linaishia kwa kipa wa JKT Tanzania
Dakika ya 51 Kaseke anapiga shuti linaokolewa na kipa wa JKT Tanzania
Dakika ya 50 Michael Aidan anapiga faulo inaokolewa na Metacha Mnata.
Dakika ya 47 JKT Tanzania wanapeleka mashambulizi kwa Yanga
Dakika ya 46 Adam anakosa nafasi ya kufunga
Kipindi cha pili kimeanza
Mapumziko
Dakika 3 zinaongezwa
Dakika ya 42 Kisinda anapiga shuti off target
Dakika ya 41 Adam Adam anapiga shuti off target
Dakika ya 39 Kisinda anachezewa faulo.
Dakika ya 37 Makapu anachezewa faulo
Dakika ya 34 Yacouba anaotea
Dakika ya 32 Goaaaaal Deus Kaseke pasi ya Yacouba Sogne
Dakika ya 30 Kaseke anaotea
Dakika ya 29 Makapu anatoa nje mpira ndani ya 18.
Dakika ya 28 Yanga wanapata faulo
Dakika ya 25 Nchimbi anakosa nafasi ndani ya 18 shuti lake linaokolewa na kipa wa JKT Tanzania.
Dakika ya 22 Jabir anachezewa faulo
Dakika ya 20 Yacouba alicheza faulo
Dakika ya 18 Kisinda alipiga faulo haikuwa na faida
Dakika ya 16 Adam Adam alipoteza mpira
Dakika 15 za mwanzo hakuna timu ambayo imeona lango.
Kipindi cha kwanzaYanga 0-0 JKT Tanzania.
Mwendo wa roho mkononi........goli moja moja watu lazime pressure ziwe juu
ReplyDeleteTimu ilipokuwa na Zahera ilikuwa haina hela ya kuwalipa wachezaji Hakuna lakini kiwango Hakuna tafauti na Yanga ya leo yenye wachezaji wa mabilioni ya shilingi na wanaposhinda ni goli mojamoja tu na kila siku tunasikia kocha keshayafanyia marekebisho. Hata kwa JKT timu ambayo imekuwa kichochoro cha timu karibu zote kujipstia ushindi wa magoli mengi mnashindwa kupata magoli mawili nanyi ndio Mabingwa wa Jadu
ReplyDeleteZlatko alipata sare moja na kushinda mechi 6. Matokeo hayo yalitosha kumfukuza kazi. Huyu Kaze tayari ana sare 3 ushinfi wa mechi ni tia maji tia maji. Tatizo ni kocha au wachezaji? Ligi inaendelea kuwa ngumu na mzunguko wa pili tutashuhudia kiama Yanga tusijidanganye
DeleteKinacho kuuma nn endeleen kufnga 7 cc yanga 2melizka na 2licho nacho na wewe endelea kupambana na hari yako
DeleteUkisoma maoni ni kwamba mdau anaitakia timu ya Yanga kuonesha mpira na matokeo walivyojinasibu kocha na viongozi na si lo lote kuhusu mikia
DeleteHuyo Jackson inaonesha anachojua ni kuangalia jinsi watu wanavyoufukuza mpira na kuupiga na wala hajui nini falsafa ya mpira,na hata aina ya uandishi wake inatosha kuonyesha kuwa ni kizazi cha miaka ya kuanzia 2005 na kuendelea.Kwa mwendo huu wa timu inatoa mwanya mkubwa kwa timu kukosa confidence ya kupata ushindi wa uhakika na pia inatoa mwanya kwa timu pinzani zisizo na uwezo kujenga confidence pindi zinapokutana na Yanga na matokeo yake inahitajika nguvu ya ziada na uwezo binafsi wa wachezaji kuweza kupata matokeo.Usije shangaa siku Yanga itakapokutana na Coastal ambayo ilipigwa goli 7 mechi inaweza kuwa ngumu kwa sababu tayari itakuwa imejengeka mentality kwa wachezaji wa Coastal kuwa uwezo wa Yanga ni mdogo na ushindi wao ni wa kubahatisha hivyo wana uwezo wa kupambana nao na kupata matokeo........huo ni mfano mdogo tu.Kupata point tatu tu sio hoja muhimu ni kupata ushindi wa uhakika ambao utakuwa unawafanya wachezaji wacheze kwa kurelax na wala sio kutumia nguvu nyingi mwanzo mwisho
DeleteEe kweli we ndo bure kabsa kwan yanga ishafnga coastal 3 ww 7 endelea kuchangia
DeleteHuo ushindi wa uhakika ni upi? Mbona ninyi mnashinda 7 bila na kuna mechi mnafungwa? Kitu kikubwa hapa ni kupata point 3 kwanza, magoli yatafuata badae. Hata mshindi anaangaliwa kwanza uongozi wa point, kama imegongana na timu byengine ndipo zinaanza kuangaliwa uwiano wa magoli. Kikubwa ni kwamba bakini na Simba yenu nasi tubaki na Yanga yetu. Kila mmoja ashinde mechi zake na pambaneni na hali yenu.
DeleteMpira magoli na point, point bila. point bila magoli Ni sawa na gari bila usukani muda wowote linapinduka
ReplyDeleteYanga inacheza na timu ngumu sio lelemama, tunashukuru ushindi
ReplyDeleteLeicester City walitwaa ubingwa wa Epl kwa staili hii, hii. Ugiriki ilitwaa ubingwa wa Euro 2004 kwa staili hii hii.Twende hivi hivi mpaka mwisho wa msimu
ReplyDelete😄😄😄 Imani yako Kali? lkn huna team yamuendelezo wa ushindi Kama hizo ulizotoa hpo juu. Unachezeshwa kwata mpaka unaomba poo na kupewa msaada na marefa. Muda cmrefu itaanza kugongwa kwa mabao mengi tu. Endelea na Imani yako mpaka mwisho uone mziki wa vpl.
DeleteManaake mnajifananisha Laicecter City. Ama kweli ulimi hauna mfupa na mnachekesha sana
ReplyDeleteKwani ninyi Mikia mnauhakika wa kushinda mechi zote? Kuna timu mnazionea na zingine zinawaonea tu kama kawaida na ndio maana mshapokea vipigo 2 vitakatifu na raundi ya 1 haijaisha. Kumbuken mnamechi nyingi huko uswazi raundi ya pili na timu zitawakazia sana kwa hofu ya kushuka daraja. Safari hii mtaongea sana mitandaoni ila ubingwa mtausikia kwenye tv na kuuangalia kwenye redio nyau nyinyi.
ReplyDelete