TIMU ya Taifa ya Tanzania chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes, kesho Novemba 30 ina kibarua cha kusaka tiketi ya kufuzu hatua ya fainali ya mashindano ya Cecafa kwa kucheza dhidi ya Sudani Kusini.
Kikiwa chini ya Kocha Mkuu, Jamhuri Kihwelo, 'Julio' kimeendelea kujiweka sawa ili kuweza kuibuka na ushindi kwenye mchezo huo utakaochezwa Uwanja wa Black Rhino, Karatu, Arusha.
Timu hiyo ilitinga hatua ya nusu fainali baada ya kushinda mechi zake zote mbili ilizocheza ambapo ilianza kwa kupata ushindi wa mabao 6-1 dhidi ya Djibout na mchezo wa pili ilikuwa dhidi ya Somalia ambapo ilishinda mabao 8-1.
Akizungumza kuhusu maandalizi, Julio amesema kuwa kila kitu kinakwenda sawa na wanaamini kwamba watafikia malengo ya kutinga hatua ya fainali na kutwaa taji la Cecafa.
Ikiwa watashinda kesho fainali watacheza Desemba 2 na mshindi kati ya mchezo wa Uganda na Kenya.
0 COMMENTS:
Post a Comment